Kila Wakati Kuwa Na Kitu Hiki

Kuwa na kitu cha kufanyia kazi. Kila wakati kuwa na namba ambayo unapaswa kuifanyia kazi. Usikubali kuwa na maisha ambayo unakuwa na muda halafu huna kitu cha kufanyia kazi. Kila wakati jipe kazi, jipe jukumu moja la kufanyia kazi na ukilimaliza jipe jukumu lingine tena. Hakuna kupoa, ni kazi kazi. Siyo kwamba usiwe na muda …

Tahadhari; Ijue Sheria Ya Mafanikio Kabla Hujapata Anguko

Waandishi Al Ries na Jack Trout kwenye kitabu chao cha THE 22 IMMUTABLE LAWS OF MARKETING wanaelezea sheria za masoko ni namna gani watu wakishapata mafanikio makubwa wanajisahau na baadaye kupata anguko. Maisha ni mauzo yaani kifupi kila kitu kwenye maisha ni mauzo sasa ili uendelee kubaki kwenye mauzo mazuri unapaswa kuwa na masoko endelevu. …

Usichukie Mafanikio Ya Wengine

Ukiona mtu anachukia mafanikio ya wengine jua kabisa hajui maana ya mafanikio kwake ni nini. Mafanikio kwako yana maana gani?Ukishajua mafanikio kwako yana maana gani huwezi kuchukia mafanikio ya watu wengine. Mafanikio yana maana tofauti tofauti kwa kila mmoja wetu. Kwa kulijua hilo usichukie mafanikio ya watu wengine bali yapende. Hakuna kitu kinawazuia watu kufanikiwa …

Usikubali Anayekuonea Aendelee Na Uonevu Wake

Kwenye maisha yako unapaswa kuwa mtu imara. Usipokuwa imara utawaruhusu watu wengine wakutawale na huwezi kuwa huru kwenye maisha yako kama umetawaliwa na mtu fulani. Kwenye maisha yako usiwe mnyonge kabisa, jiamini, na simamia kile unachokiamini. Kama unaishi bila kuvunja sheria za asili, nchi na kanuni za maadili huna cha kuhofia. Bali ishi kwa uhuru …

Tafakari Ya Kumbukizi Yangu Ya Kuzaliwa, Kitabu Kipya; SHOW ME THE WAY, NIONESHE NJIA NA ZAWADI

NAJIWASHA MOTO NJOONI MNIONE NIKIUNGUA Habari rafiki yangu nikupendaye, Leo Julai 18, ninaadhimisha kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa hapa duniani. Nilizaliwa miaka 33 iliyopita. Kwa namna ya pekee kabisa namshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha kwa kunistahilisha kusimama mbele yake na kuendelea kumtumikia na hatimaye leo naadhimisha kumbukumbu yangu ya kuzaliwa. Mwaka jana nilifanya …

Matashi Mema Aliyoniandikia Rafiki Yangu Kwenye Kumbukumbu Ya Kuzaliwa Kwangu

Rafiki yangu, Leo ni siku yangu ya kuzaliwa, katika maamuzi magumu ambayo nimewahi kufanya kwenye maisha yangu mwaka huu basi ni kuachana na ajira. Ni maamuzi sahihi kwangu na leo nayafurahia, sijui nilipata wapi nguvu hiyo lakini namshukuru sana Mungu kwa kunipa nguvu za ajabu za kuachana na ajira. Huwa nafanya sana tafakari ya maisha …

Kama Unataka Kwenda Mbinguni Epuka Kufanya Dhambi Hizi Hapa Mbili

Siko hapa kukuhubiria injili bali niko kukuambia vitu viwili tu ambavyo vinawakwamisha watu wengi kufanikiwa kwenye maisha yao. Hata kwenda mbinguni ni mafanikio pia lakini siyo kila mtu ataenda mbinguni kwa sababu ya yale anayofanya. Tabia ulizonazo na yale unayofanya unafikiri yatakufikisha kule unakotaka kufika? Acha utani, weka kazi hakuna kitu kirahisi. Ingekuwa rahisi kila …

Naweza Kuajiri Watu Kunisaidia Kufanya Kila Kitu, Isipokuwa Vitu Hivi Viwili

Frank Bettger katika kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling aliweza kumnukuu na kujifunza kauli moja kutoka kwa aliyekuwa mmiliki wa viwanda alisema hivi, naweza kuajiri watu kunisaidia kufanya kila kitu isipokuwa vitu viwili tu, kufikiri na kufanya vitu kwa mpangilio wa umuhimu wake. Rafiki yangu, huwa nakushirikisha hapa vitu …

Vitu Viwili Muhimu Vya Kuzingatia Kwa Kila Muuzaji

Ni imani yangu kwamba kama uko hai, basi kuna kitu unaendelea kuuza hapa duniani. Kwa sababu hakuna mtu ambaye anaweza kuendesha maisha yake pasipo mauzo. Tunapouza maana yake tunatoa, na katika maisha asiyetoa maana yake hapokei, hivyo basi, kila anayetoa huwa anapokea kadiri ya sheria ya asili. Ukiwa kama muuzaji bora kuwahi kutokea kwenye eneo …

Kitu Ambacho Huwezi Kukibadilisha Kwenye Mahusiano

Kuna wakati huwa tunaumia kwenye mahusiano yetu kwa sababu ya kujitakia wenyewe. Kwenye mahusiano, watu wengi wanapenda kuwa viranja wa kuwatawala wengine, yaani wanataka watu wengine waishi kama vile wanavyotaka wao. Kitu ambacho huwezi kukibadilisha kwenye mahusiano ni kumbadilisha mtu kuwa kama vile unavyotaka wewe. Ni kazi kubwa sana, pata picha mtu amekulia malezi tofauti, …

Design a site like this with WordPress.com
Get started