Design a site like this with WordPress.com
Get started

Aina Mbili Za Ujasiri Unazopaswa Kuwa Nazo Ili Ufanikiwe

Wengi wanatamani kuwa na mafanikio lakini cha ajabu hawana ujasiri wa kufikia ndoto zao.

Bila kuwa na ujasiri ni ngumu sana kufanikiwa.

Ujasiri ni kuweza kutenda licha ya kuwa na hofu. Ujasiri siyo kutokuwepo kwa woga. Kiasili kila binadamu huwa na hofu na woga pale anapotaka kufanya jambo jipya, sasa kitendo cha kuthubutu bila kujali hofu au woga wa mtu ndiyo tunaita ujasiri.

Ujasiri ni kuwa mkubwa kuliko matatizo yako yanayokuandama. Unapokuwa na matatizo unajiona wewe ni mkubwa kuliko tatizo lenyewe, jione kama vile uko juu ya anga na unaiona dunia ilivyokuwa ndogo.

Shabaha yetu ya leo kujua aina mbili za ujasiri ambazo mtu akiwa nazo zitamwezesha kufanikiwa.

Moja ni ujasiri wa kuanza kuchukua hatua. Watu wengi hawajiamini ndiyo maana hawana ujasiri wa kuchukua hatua.

Ili ujenge ujasiri huu wa kuchukua hatua, unapaswa kuanza kujiamini wewe mwenyewe kwanza kwamba unaweza kufanya makubwa kwenye kile unachotaka kufanya.

Mbili ni ujasiri wa kuendelea kutenda. Ili uwe na ujasiri huu unapaswa kuwa na hamasa au hamu ya kutaka kufanikiwa.

Bila ya kuwa na hamu ya kutaka kufanikiwa ni rahisi sana kuishia njiani.

Pata picha pale mtu unapokuwa una hamu ya kitu fulani unakua unajituma mpaka upate kitu hicho ili hamu yako iishe.

Kuwa na hamu ya mafanikio utapata ujasiri wa kuendelea kutenda.

Hatua ya kuchukua leo; unahitaji ujasiri wa aina mbili ili uweze kufanikiwa, moja kuwa na ujasiri wa kuchukua hatua na kutenda na mbili kuwa na ujasiri wa kuendelea kutenda.

Rafiki yangu, jitoe kwenye ujasiri huo na utakuwezesha kupata kile unachotaka.
Ni ngumu sana kuonekana kwenye kitu chochote kile kama hutaweka juhudi hizo mbili.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505//0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: