Njia Wanayotumia Wateja Wengi Kukutoroka

Kwa kuwa wewe ni muuzaji bora kuwahi kutokea, unapaswa kuwa vizuri sana kwenye eneo la mauzo kwani mauzo ndiyo yanaleta fedha mifukoni. Hakuna watu wajanja kama wateja, wanazo mbinu nyingi wanazotumia pale wanapokuwa hawataki kununua kwako. Na siyo kwamba hawana hela, hela wanazo na wakiamua kukupiga chenga wanakujibu jibu ambalo halitakufanya uumie. Wateja wanajua sisi …

Tatizo Lako Linatatuliwa Na Fedha?

Ukijaribu kuchunguza changamoto nyingi ambazo watu wanakabiliana nazo zinatokana na kukosa fedha za kutatua changamoto zinazowakabili. Kama una changamoto na ukipata fedha unaweza kuitatua basi wewe hapo changamoto yako ni kwamba huna fedha ya kutatua changamoto zinazokukabili. Kama fedha inaweza kutatua changamoto uliyonayo, basi pambana uweze kupata fedha zaidi. Mwandishi na mfanyabiashara Kevin O’Leary anasema …

Nilichojifunza Kwenye Haya Maisha

Pale tunapokutana na changamoto au mambo hajaenda kama vile tunavyotaka sisi huwa kitu cha kwanza tunachofikiria ni nani amesababisha lakini huwa tunajisahau na sisi tumehusikaje kutokea kwa kile kilichotokea. Hata sisi wenyewe huwa tunachangia sana kwa changamoto mbalimbali katika maisha yetu lakini huwa hatukubali tunajiona sisi ni watakatifu. Kwenye kila kitu kinachotokea kaa chini jiulize …

Utabana Matumizi Mpaka Lini?

Ukitaka kuiona hela ongeza kipato na punguza matumizi yasiyokuwa na ulazima kwenye maisha yako. Ni kweli utapunguza sana matumizi lakini kuna matumizi mengine hata upunguze vipi bado ni muhimu sana. Ili maisha yako yaende lazima ufanye matumizi hayo. Yako matumizi yasiyokuwa na ulazima na yako ambayo yanaulazima, huwezi kuyaacha kwa sababu bila hayo maisha yako …

Haya Ndiyo Maisha Ya Furaha

Watu wengi huwa wanapenda kujiingiza katika maisha ya msongo kwa kununua matatizo ya kujitakia. Huwa tunahangaika na mambo mengi ambayo yako nje ya uwezo wetu ndiyo maana tunakosa furaha. Tukishindwa kuyadhibiti basi tunakuwa na maisha ya msongo. Mwanafalsafa wa ustoa, Epictetus anasema maisha ya furaha ni pale unapojua kile ambacho kipo ndani ya uwezo wako …

Miaka 6 Ya Kuandika Kila Siku Na Mambo Kumi Ya Kujifunza

Ilikuwa ni tarehe moja mwezi octoba mwaka 2016 ndipo nilianza marathoni ya kuandika kila siku bila kuacha. Namshukuru Mungu kwa yote katika kipindi chote cha miaka 6 ya kuandika kila siku. Yako mengi ambayo unaweza kujifunza kupitia kazi yangu ya uandishi. Kuandika ni kazi kama zilivyo kazi nyingine lakini ni kazi ngumu kwa sababu inahitaji …

Kama Umepanda Gari Sahihi

Unapata wasiwasi gani wa safari? Kwa mfano, umepanda gari lako la kwenda Arusha, lakini ukiwa kwenye gari unaanza kujiuliza sasa mbona Arusha hatufiki? Kama umepanda gari sahihi usiwe na wasiwasi utafika kule unakokwenda. Hii ina maana kwamba, ukikaa kwenye mchakato sahihi wa kufanya kitu fulani usiwe na wasiwasi na matokeo. Kwa sababu matokeo mazuri yatakuja …

Tunza Uadilifu wako

Uadilifu ni kuishi kile ulichoahidi na unachosimamia kwa mfano, umeahidi utakua mwaminifu katika maisha yako. Basi unaishi kile ambacho umekiahidi na ukienda kinyume maana yake umevunja uadilifu wako. Uadilifu wako una thamani kubwa kuliko almasi hivyo basi, usifanye chochote kile cha kuharibu uadilifu wako kwa sababu ukishauchafua ni vigumu kuusafisha. Umekula kiapo cha kuwa mwaminifu …

Ulishawahi Kukutana Na Hali Hii Ukipata Fedha?

Iko wazi kwamba, kuna watu ambao wakipata fedha zinakuwa zinawawasha yaani wanakuwa hawawezi kutulia nazo mpaka ziishe. Kwa sababu watu wengi wanakutana na hali hii, leo nataka kukusaidia kupata suluhisho lake. Kama unapata fedha na huwezi kutulia nazo ni rahisi watu kukujua na kukulaghai wanapojua una fedha. Suluhisho la hili rafiki yangu nikupendaye, unapaswa kujijengea …

Njia Rahisi Ya Kuwapoteza Wateja Wako

Uwe unafanya biashara au hufanyi lakini kiasili kila mtu ana mteja wake kwa sababu kuu moja ambayo ni kila mtu ni muuzaji. Kwa sababu kama huna unachouza utayaendeshaji maisha yako? Wako wanaouza huduma, ujuzi, maarifa, uzoefu, muda nk. Kitu muhimu sana wewe kama muuzaji unachotakiwa kufanya ni kutimiza ahadi unazotoa. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanawadanganya wateja …

Create your website with WordPress.com
Get started