Waandishi Al Ries na Jack Trout kwenye kitabu chao cha THE 22 IMMUTABLE LAWS OF MARKETING wanaelezea sheria za masoko ni namna gani watu wakishapata mafanikio makubwa wanajisahau na baadaye kupata anguko.
Maisha ni mauzo yaani kifupi kila kitu kwenye maisha ni mauzo sasa ili uendelee kubaki kwenye mauzo mazuri unapaswa kuwa na masoko endelevu. Kwa mfano, umepata mafanikio kwenye kazi, biashara nk, hupaswi kuweka mikono mifukoni bali unapaswa kuendelea kujifunza na kuchukua hatua kama vile ndiyo unaanza. Lakini watu wakishapata mafanikio kidogo wanajisahau na baadaye kupata anguko.
Mafanikio huwa yanaleta kiburi na kiburi huwa kinaleta kushindwa.
Watu wanapofanikiwa huwa wanajiona wameshajua kila kitu, wanaacha kuweka juhudi walizoweja mwanzo na wanaanza kushindwa.
Haijalishi umefanikiwa kiasi gani, epuka sana kuwa na kiburi, epuka sana kujiona umeshajua kila kitu.
Henry Ford aliwahi kunukuliwa akisema, haijalishi umri wako ni miaka 20 au 80, kama hujifunzi unakuwa mzee.
Hatua ya kuchukua leo; kila siku na kila wakati endelea kujifunza na kuchukua hatua kama vile ndiyo unaanza.
Haijalishi umefanikiwa kiasi gani, kuwa mnyenyekevu na usiwe na kiburi kwa sababu kiburi huwa kina tabia ya kunyang’anya mafanikio uliyonayo.
Jifunze na usiwe na kiburi kwa sababu chochote kile ambacho unacho kwenye maisha yako.
Chochote ulichopewa kitumie kwa hekima na unyenyekevu na si vinginenvyo.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog