Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndio Tofauti Kubwa Kabisa Kati Ya Kusikia Na Kusikiliza

Habari mpendwa Rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo ? natumaini unaendelea vizuri rafiki yangu na karibu katika makala yetu ya leo ambapo leo tutajifunza kwa pamoja tofauti kubwa kati ya kusikia na kusikiliza.
Dunia ya sasa imejaa kelele nyingi. Na changamoto kubwa ni kupata mtu wa kukusikiliza kwani watu wengi wako bize na mambo yao ya kila siku. Kusikiliza ni kazi ngumu ambayo inawashinda watu wengi sana. Kumekuwa na desturi ya mtu kuongea bila hata ya kukaa kimya na kumsikiliza mwenzake amalize kuongea. Kuongea ni rahisi kuliko kusikiliz na tunashauriwa kwamba tuwe wasikilizaji bora kwani tutajifunza mambo mengi sana kuliko ukiwa muongeaji. Kusikiliza ni sayansi ambayo inahitaji kuhusisha mwili na akili vyote kwa wakati mmoja. Na kama ulikuwa hujui ndugu rafiki kuna tofauti kubwa kati ya kusikiliza na kusikia.
Kusikia (hearing) ni nini? Ni uwezo wa asili wa kupokea mawimbi ya sauti au jumbe. Kwa mfano, labda wewe uko darasani unasoma na mwalimu yuko mbele ya ubao anafundisha halafu unasikia nje sauti za magari, ndege na sauti mbalimbali huko nje wakati wewe ukiwa darassani hiyo ndiyo tunaita kusikia (hearing). Kusikia ni kitu ambacho kina kuja tu kiasili wala huwezi hata kukizuia kama vile wewe unaweza kujizuia kupiga chafya? Kukoa? Kwahiyo huwezi kujizuia kusikia, unasikia lakini unakuta akili yako na mwili wako haviko pale. Kwa mfano rafiki yangu hapo ulipo sasa umekaa unasoma makala hii akili yako na mwili wako umevielekeza katika kusoma makala hii lakini husikii watu,au sauti za vitu mbalimbali huko nje au pembeni yako? Sasa hiyo ndio maana ya halisi ya neno kusikia rafiki yangu.
Rafiki, mpaka sasa umeshajua nini maana ya kusikia. Je kusikiliza (listening) ni nini? Ni mchakato wa kuchagua nini cha kusikia kwa ajili ya kuelewa jambo Fulani kwa dhumuni la tukio au shughuli Fulani.

Kusikiliza ni kukusudia (intentional) una uwezo wa kuamua kusikilza au kutokusikiliza. Kusikiliza inahusisha ujuzi ambao mtu anaweza kujifunza au kufundishwa. Kwa mfano, mwanafunzi darasani anasikiliza ili aweze kupata maarifa. Katika mahakama hakimu anasikiliza maelezo ya pande zote mbili kutoka kwa shahidi,mtuhumiwa na mawakili ili aweze kufanya hukumu.
Kwahiyo,kuna tofauti kati ya kusikia na kusikiliza. Kuna muda mwingine tunasikia hata kama hatuko tayari kusikia kwa mfano, fikiria kelele zinazopigwa pale unapotaka kulala. Lazima utapokea mawimbi ya sauti kwasababu unauwezo wa kusikia. Tunafanikiwa kusikia kwasababu sisi siyo viziwi. Na kusiliza ni kitu kitu ambacho una hiyari nacho kusikia au kutosikiliza yaani una maamuzi ya kufanya. Kusikiliza ni kazi kuliko kusikia. Anza kuwa msikilizaji bora kuanzia leo.
Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Join the Conversation

1 Comment

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: