Habari ya leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa KESSY DEO? Ni imani yangu kuwa uko vizuri na unatumia vizuri uwepo wako hapa duniani.
Kama nilivyokushirikisha hapo awali kuwa tarehe moja ya mwezi wa kumi nilitimiza mwaka mmoja wa kuandika kila siku kupitia mtandao huu wa Kessy Deo. Hivyo basi, tokea nianze safari ya kuandika 2014 mpaka leo nimekuwa naombwa na wasomaji wengi kuanzisha kundi. Wengi wananiuliza nina kundi ninawajibu hapana bado sijaanzisha kundi na lengo langu ni kutaka kwanza mimi mwenyewe kuwa vizuri na kujingea nidhamu binafsi.
Huwezi kubadilisha watu kama wewe mwenye huna nidhamu ya kitu chochote kile hivyo kwani unaweza kuibadili dunia yako kwa kujibadili wewe mwenyewe kwanza. Hivyo kwa sasa niko tayari kuanzisha kundi katika mtandao wa wasapu ambao katika kundi hili tutaweza kuwa pamoja zaidi. Natumaini tokea uanze kusoma hapa ndani ya mwaka mmoja lakini pia kama ulishaanza kunisoma kupitia mtandao wa Amka Mtanzania na amini kuwa umeweza kuiona thamani yangu ni ipi na utakuwa unanifahamu vizuri misingi na falsafa yangu.
SOMA; Habari Njema Kwako Rafiki Na Msomaji Wa Mtandao Wa Kessy Deo
Nimeandaa utaribu mzuri sana katika kundi nililolianzisha hivyo ukijiunga utakwenda kufurahia huduma nzuri sana. Rafiki kama unavyojua kuandaa makala mpaka inakufikia wewe hewani ninatumia gharama kubwa na kila siku unapata kusoma hapa bila sababu hivyo kupitia kundi hili la wasapu utakuwa unapata kitu cha ziada ambacho ulikuwa hukipati katika makala za kawaida kila siku lakini utapaswa kuchangia gharama kidogo ambacho ni kiwango kidogo kitakachokuwa ndani ya uwezo wako.
Kwahiyo, mambo muhimu utakayokuwa unanufaika nayo ni kama ifuatavyo;
Jina la kundi au klabu yetu itakuwa inaitwa MIMI NI MSHINDI, NIMEZALIWA KUSHINDA (I AM THE WINNER, BORN TO WIN)
- Nukuu fupi zilizobeba hamasa ndani yake yenye tafakari ya kuanza siku yako ukiwa chanya.
- Uchambuzi wa kitabu kila wiki.
- Makala mpya kila siku.
- Nafasi yangu leo ya kuwa mwalimu. Hii ni sehemu ambayo kila mwanachama anaalikwa kuwa mwalimu kwa kupewa nafasi yake ndani ya siku husika au muda husika. Hapa mwanachama atapata nafasi ya yeye kuweza kufundisha au kushirikisha mwanachama mwenzake kile anachojua au anachofanya kadiri ya kazi yake, uzoefu wake na hata ujuzi ambao anao ili kutanua wigo wa maarifa na watu kujifunza na kuchukua hatua.
Kila mtu ana kitu cha kipekee cha kushirikisha dunia ambacho mtu mwingine hana kitu hicho hivyo ukiwa katika kundi la MIMI NI MSHINDI, NIMEZALIWA KUSHINDA utapata nafasi ya kushirikisha kile unachojua. Na katika kipengele hiki cha nafasi yangu kuwa mwalimu kitakuwa kinafanyika kila mwisho wa juma yaani jumamosi au jumapili.
- Pia, utapata nafasi ya kutafakari siku yako ilikwendaje ndani ya siku husika, kwanini unatakiwa kufanya hivyo? Kwa sababu mwanafalsafa plato aliwahi kusema maisha ambayo hayachunguzwi au hayatathiminiwi ni maisha ambayo hayana maana kuishi hivyo basi maisha yako yatakuwa na maana kwa kushirikisha kile ulichojifunza kwa mwenzako.
- Kwahiyo, utaanza siku yako kwa ushindi na kumaliza siku yako kwa ushindi huku ukiwa na hamasa kubwa ya kwenda kuanza siku inayofuta. Ushindi wowote siku zote huwa unaongeza ushindi hivyo ushindi utakaokuwa unapata kila siku utabadili maisha yako kiroho, kimwili na kiakili.
Rafiki , napenda kukualika sana katika kundi hili letu jipya la mtandao wa Kessy Deo, karibu uonje utofauti, karibu tunufaike wote kwa pamoja.
JINSI YA KUJIUNGA NA KUNDI HILI;
Kujiunga na kundi hili kwa mara ya kwanza ni shilingi elfu tano tu na kupatiwa zawadi ya kitabu miongoni mwa vitabu nilivyoandika mimi. Utachagua miongoni mwa kitabu mojawapo kati ya hivi FUNGA NDOA NA UTAJIRI, KWANINI MSAMAHA NA ONGEA LUGHA YAKO ( SAUTI YAKO YA NDANI NDIYO MAFANIKIO YAKO, SIKILIZA SAUTI YAKO YA NDANI, NGUVU YA KUSUDI LA MAISHA YAKO HAPA DUNIANI)
Rafiki, kuna marafiki zangu wengi ambao tayari walishanunua miongoni mwa vitabu hivyo hapo wao hawatalipia kiasi hicho cha shilingi elfu tano badala yake wao watatakiwa kulipia kiasi cha shilingi elfu tatu.
MUHIMU; ADA YA KUNDI HILI KWA MWEZI NI ELFU TATU, HIVYO KAMA UTAKUA UMELIPIA TAREHE 17/10/ hivyo utatakiwa kulipia tena ada hiyo tarehe kama hiyo ya mwezi wa kumi na moja au ujao.
Kama utapenda kulipia kwa kwa mwaka utalipia elfu thelatini tu na kama hutoweza kulipia kwa kwa pamoja basi unakaribishwa kulipa kwa mwezi ambayo ni elfu tatu, elfu tatu kwa mwezi ni sawa na shilingi mia kila siku hivyo kwa shilingi mia ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako na ambaye yuko tayari hawezi kuwa na sababu tena.
JINSI YA KUTUMA MALIPO; TUMA MALIPO KWA MPESA 0767101504 AU TIGO PESA NA AIRTEL MONEY KWA NAMBA 071710150, BAADA YA KUTUMA MALIPO , TUMA MAJINA YAKO KUPITIA WASAPU NAMBA 0717101505 NA UTAUNGANISHWA.
Rafiki, karibu sana katika kundi letu jipya la mtandao wetu wa Kessy Deo. Kila la heri rafiki yangu.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505/0767101504