Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usiongeze Chumvi

Kwenye mchakato wa mauzo , unaweza ukasema ni bora uongeze chumvi kidogo ili uweze kumnasa mteja.Kuongeza chumvi yaani kusema maelezo ambayo hata hayapo ni njia rahisi kabisa ya kumfukuza mteja kirahisi. Ongea ukweli, hata kama upande wa pili hawajui wewe ukishajua nao watakuja kujua. Kuongeza chumvi, kutakupotezea wateja wako wote na mtu akigundua kwamba uliongeza …

Jinsi Ya Kukabiliana Na Mteja Mjuaji

Kwenye mchezo wa mauzo huwa tunakutana na wateja wengi, kazi yako kubwa kama mtu wa mauzo ni kuweza kukamilisha mauzo. Haijalishi umepiga chenga nyingi kiasi gani kama hujakamilisha mauzo unakua huna ulichofanya. Kwa nini tunasisitiza zaidi mauzo kwa sababu mauzo ndiyo moyo wa na fedha ndiyo damu ya biashara. Kama mtu hana moyo wala damu …

Hii Ndiyo Huduma Unayopaswa Kumpa Mteja Wako

Kipimo kizuri cha huduma bora kwa mteja ni kujipima kwa sentensi hii”Mara zote nitampa mteja huduma ambayo mimi mwenyewe ningejipa kama ningekuwa mteja huyo” Kuna wakati tunawahudumia wateja wetu lakini hatuwapatii huduma bora. Na watu wengi hawatoi huduma bora ndiyo maana hawafanikiwi. Watu wanaangalia wanapataje fedha kabla hawajaangalia wanasaidiaje kwa kutoa huduma bora. Mafanikio yoyote …

Huyu Ndiyo Muuzaji

Kila mtu ni muuzaji.Muuzaji ni yule anayemshawishi mwenzake. Kitendo cha wewe kuweza kumshawishi mwenzako kukubaliana na wewe huo ni uuzaji. Siyo lazima anunue bidhaa, ila hata kukubaliana na wewe tu kimawazo ni uuzaji.Uuzaji ni kitendo cha kubadilishana imani. Kifupi, uuzaji ni mbadilishano wa imani, mmoja anamshawishi mtu ili aweze kukubaliana na kile anachokiamini.Ukisema wewe siyo …

Utawashawishi Watu Kwa Kitu Hiki

Njia nzuri ya kuwashawishi watu kwenye maisha yako ni kuwashawishi kwa matokeo. Matokeo yana nguvu kubwa ya kumfanya mtu akubaliane na wewe kirahisi. Kama wewe ni muuzaji, ukitaka kuwashawishi watu wakubaliane na wewe kwenye kile unachouza, waonyeshe matokeo wanayokwenda kuyapata. Watu wanaamini sana kwenye matokeo kuliko kitu chochote kile. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu …

Kitu Kimoja Kinachomfanya Muuzaji Ajisikie Vizuri

Kwenye mauzo, muuzaji kama hauzi, anakuwa anajisikia vibaya. Siyo tu kujisikia vibaya lakini pia kukata tamaa na kuona kama vile hana bahati au ana kisirani. Lakini muuzaji anajisikia vizuri pale anapokuwa anauza. Kitu ambacho naweza kukuambia ni kwamba, kuuza ni raha. Kuuza raha kwa muuzaji wowote yule, mtu anapokuwa anauza na anaona mauzo anapata hata …

Waambie Watu Kitu Hiki

Kuna wakati unaweza kujiona kama vile dunia ina kisirani na wewe lakini ukija kuchunguza utakuja kugundua kwamba tatizo siyo dunia bali tatizo ni sisi wenyewe kwa kushindwa kukaa kwenye mchakato wa kile tunachotaka. Watu wengi wana bidhaa, wana kitu ambacho wanakiuza lakini watu hawajui kama wanauza. Wanalalamika hawauzi siyo kwamba wateja hakuna tatizo biashara haijulikani. …

Wateja Wengi Hawapendi Hiki Kitu

Wateja wanapenda kununua na siyo kuuziwa. Hii ina maana gani? Kuuziwa ni pale ambapo unataka kumuuzia kitu mteja bila kumuonesha thamani. Ni pale unapokuwa na kitu unamuomba mteja akuungishe. Tunasahau kwamba wateja hawanunui kwa kukuonea huruma, bali wateja wananunua kwa sababu zao binafsi. Kwani wewe vitu ulivyonunua jana ulinunua kwa sababu ya mteja au kwa …

Wauzie Watu Kitu Hiki

Wauzie watu kile ambacho watu tayari wanataka. Usijisumbue kuwauzia watu kitu ambacho hawakitaki. Huko ni kupingana na asili. Ni kupingana na soko, mara zote soko huwa halina huruma hivyo linampiga yeyote anayekwenda kinyume na soko. Kwa mfano, ulaji wa vitoweo, huhitaji nguvu KUBWA kumshawishi mtu kula kuku.Lakini, Unahitaji nguvu KUBWA kumshawishi mtu kula kware. Hapo …

Aina Mbili Za Ushindi Kwenye Mauzo

Mpendwa muuzaji, Kila mtu ni muuzaji, iwe umejiajiri au umeajiriwa basi wewe ni muuzaji kwa sababu kupitia mauzo ndiyo yanafanya maisha yako yaweze kwenda. Kwenye mauzo kuna ushindi wa aina mbili, Moja, kuuza.Kwenye kuuza hapa ni pale mteja anapotoa hela yake mfukoni na kununua kile unachouza. Mbili, kuuziwa. Kuuziwa ni pale mteja anapokupa sababu ya …