Kuna wakati huwa tunaumia kwenye mahusiano yetu kwa sababu ya kujitakia wenyewe.
Kwenye mahusiano, watu wengi wanapenda kuwa viranja wa kuwatawala wengine, yaani wanataka watu wengine waishi kama vile wanavyotaka wao.
Kitu ambacho huwezi kukibadilisha kwenye mahusiano ni kumbadilisha mtu kuwa kama vile unavyotaka wewe.
Ni kazi kubwa sana, pata picha mtu amekulia malezi tofauti, mazingira tofauti na ameshajijengea tabia zake halafu wewe unataka umbadili ndani ya muda mfupi.
Kitu ambacho nimejifunza ni kwamba, ukikazana kumbadilisha mtu awe kama vile unavyotaka wewe ndiyo kama unamchochea azidi kuzidisha tabia aliyonayo ambayo wewe huipendi.
Usijipe kazi ya kutaka kumbadilisha mtu, kazi yako kubwa katika mahusiano uliyonayo kwa wale ambao unahusiana nao ni kuwakubali jinsi walivyo na kunufaika nao kwa yale mazuri kutoka kwao.
Ukisema upambane na madhaifu ya mtu, utajikuta unagombana na kila mtu. Kila mtu utamwona hastahili kwako, na ni kazi sana duniani kukutana na mtu ambaye changamoto yoyote ile.
Hatua ya kuchukua leo; usikazane kuwabadilisha watu, nenda nao kadiri ya jinsi walivyo wao.
Angalia mazuri ya mtu na kisha endelea kunufaika naye kwa mazuri ambayo anayo, ukitafuta mabaya tegemea kuyapata.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog