Ikiwezekana Kaa Mbali Kabisa Na Watu Hawa

Kuna watu ambao kila ukienda kwao na wazo la kufanya kitu cha tofauti, hata kabla hawajakusikiliza unapanga utafanyaje, tayari wanakuwa na jibu kwamba haiwezekani. Kaa mbali na watu ambao wanakuambia haiwezekani. Watu wa haiwezekani hawana maana kwenye hii dunia zaidi ya kuwaaminisha wengine kwamba mambo hayawezekani kumbe yanawezekana. Watu wa haiwezekani, ni watu ambao unapaswa …

Usimpe Mtu Ahadi Ya Kuendelea Kutegemea Wakati Huna Uhakika Wa Kumpatia

Kwenye jamii zetu watu wamekuwa ni mabingwa wa kutoa ahadi na inafikia mahali ahadi zinawafunga watu na hata kukosa raha kwa sababu kila akiangalia amezungukwa na ahadi nyingi alizoamua kuahidi kwa hisia. Maisha ni yako na una uamuzi wa kutoa pale unapojisikia kutoa na siyo lazima. Usijifunge na ahadi, kama kitu huna uwezo nacho kutoa …

Usiwe Kopo Linaloelea Juu Ya Maji Likiwa Limefungwa

Ukichukua kopo la maji au chupa ya maji halafu ukaifunga na kuitupia kwenye mto, bahari, au ukaiweka bombani ikiwa imefungwa kamwe maji hayawezi kuingia ndani. Hii ina maana gani katika maisha yetu ya kawaida? Watu wengi huenda wanafanya kile wanachopaswa kufanya lakini hawapati matokeo mazuri yanayofanana na juhudi wanazoweka. Yaani wako kwenye maji lakini hawayafaidi …

Ukiwa Na Hali Hizi, Epuka Kufanya Maamuzi

Kwenye kitabu cha the Baron letters kilichoandikwa na mwandishi Gary Halbart,  anamshirikisha  mtoto  wake  makosa  ambayo  amewahi kuyafanya kwenye  maisha  yake,  na  mengi aligundua  aliyafanya  akiwa  kwenye  moja  ya  hali  hizi nne.  Hivyo  anamwambia  mtoto  wake  asifanye  maamuzi  yoyote anapojikuta  kwenye moja  ya  hali  hizo  nne; Moja; hasira. Usifanye maamuzi ukiwa kwenye hasira, jisubirishe kufanya …

Jinsi Ya Kuongeza Kiwango Chako Cha Utambuzi

Je, unajua kiwango chako cha utambuzi? Kabla hujaongeza kiwango chako cha utambuzi, unapaswa kwanza kujua au kupima kiwango chako cha utambuzi kikoje. Njia ya kupima kiwango chako cha utambuzi ni kwenye kujua majira ya siku.Hapo inakuwaje sasa?Ni rahisi sana, kwa mfano, bila ya kuangalia saa, sema muda ni saa ngapi yaani sema saa na dakika. …

Jinsi Ya Kuondokana Na Wivu

Maana rahisi ya wivu ni kujiona wewe unastahili zaidi kuliko wengine. Sina uhakika kama itakufaa, na wivu ni wivu tu, hakuna wivu mzuri wala mbaya. Jinsi gani ya kuondokana na wivu? Usiwe na wasiwasi utapata majibu sahihi hapa. Kwanza ni rahisi sana, usijilinganishe na yeyote. Pili, kubali kwamba kuna watu watakaokuwa wamekuzidi kwa chochote unachofikiri …

Pata Picha Leo Unaacha Kuwa Hivi

Kama ulikuwa haujui, akili zetu sisi binadamu ni volkano ya maoni. Kwa nini? Kwa sababu tunapenda kuwa na maoni kwenye kila kinachotokea aidha tunakijua au hatukijui ndiyo maana ukiwaomba watu maoni hata hana atajilazimisha kusema tu maana asipofanya hivyo watu watamuonaje au watamchukuliaje. Wanafalsafa wengi wanatuambia siyo sahihi kuwa na maoni kwenye kila kitu. Kama …

Usitafute Huruma Kwa Watu Wengine

Ni kawaida yetu sisi binadamu pale tunapopitia changamoto mbalimbali zinazotukabili huwa tunaona ni vema na haki kutafuta huruma kwa watu wengine juu ya yale tunayopitia. Tunafikiri kwamba, kwa njia ya kuwaelezea wengine matatizo yetu ili watuhurumie ndiyo tunaweza kutatua tatizo. Pambana na hali yako, usitafute huruma kwa watu, kila mtu ana changamoto zake hivyo yakabili …

Naweza Kuajiri Watu Kunisaidia Kufanya Kila Kitu, Isipokuwa Vitu Hivi Viwili

Frank Bettger katika kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling aliweza kumnukuu na kujifunza kauli moja kutoka kwa aliyekuwa mmiliki wa viwanda alisema hivi, naweza kuajiri watu kunisaidia kufanya kila kitu isipokuwa vitu viwili tu, kufikiri na kufanya vitu kwa mpangilio wa umuhimu wake. Rafiki yangu, huwa nakushirikisha hapa vitu …

Hiki Ndiyo Kinaathiri Maisha Yako

Dunia inatufundisha vitu vingi, kwa kuona, kusikia na kwa kufanya. Asili huwa inatufundisha vitu vingi sana katika maisha lakini changamoto kubwa ya watu wengi hawajui namna ya kukielewa kile ambacho asili huwa inawafundisha. Ruben Gonzalez aliwahi kunukuliwa akisema, kinachoathiri maisha yako siyo kinachotokea, bali jinsi unavyopokea na kufanyia kazi kinachotokea. Nakubaliana na Ruben Gonzalez kwa …

Create your website with WordPress.com
Get started