Design a site like this with WordPress.com
Get started

KITABU; JIPATIE NAKALA YA KITABU CHA MABADILIKO 250 YA USHINDI

Habari ya leo mpendwa rafiki?

Ni imani yangu hujambo na unaendelea vizuri. Hongera sana kwa juhudi mbalimbali unazoweka kuhakikisha unapiga hatua kwenda mbele.

Ili tuweze kufanikiwa kwenye kitu chochote lazima tufanye mabadiliko ya kweli. Hata kama unataka kuwa vizuri kiakili lazima ufanye mabadiliko kwanza ya akili, kama ulikuwa ni mtu ambaye huna maarifa chanya unayoingiza katika akili yako basi ukianza kufanya mabadiliko ya kuanza kusoma tu vitabu basi utakua kiakili bila hata ya wewe mwenyewe kutegemea.

Image may contain: 1 person
PATA NAKALA YA KITABU HIKI KWA SHILINGI ELFU KUMI. TUMA MALIPO KWENDA NAMBA 0717101505/0767101504 NA TUMA NA EMAIL YAKO UTATUMIA KITABU. KARIBU SANA RAFIKI.

Tunahitaji mabadiliko mengi katika maisha yetu ili tuweze kusogea na siyo kubaki hapo hapo ulipo kila siku. Tunahitaji mabadiliko ya kiroho, kiakili na hata kimwili. Mafanikio yetu yote tunayotafuta yamegawanyika katika maeneno hayo matatu ambayo ni maeno ya kiakili, kiroho na kimwili. Hata ukisema ubadilike kimwili na uwe vizuri bado utakua una utupi ndani yako, ndiyo maana katika mafiga jikoni yanakuwa matatu kwa sababu bila mafiga matatu huwezi kupika.

Tunahitaji mabadiliko kweli katika maisha yetu kwa sababu mabadiliko huwa yanatuletea fursa katika maisha yetu. Faida kubwa na sifa moja wapo ya mabadiliko ni huwa mabadiliko  huwa hayamwachi mtu kama alivyo. Uwe unataka au hutaki kubadilika lakini mabadiliko yatakuathiri tu kwa namna moja au nyingine. Miili yetu huwa inabadilika kulingana na hali ya hewa ya mahali husika, kama ukiwa sehemu ya baridi basi na mwili unabadilika kadiri ya mazingira na hali ya hewa na unajiandaa kukabiliana na kama ni baridi au hali joto.

Mabadiliko ya kweli huwa yanaleta mafanikio ya kweli. Unapoanza kufanya mabadiliko ya ndani huwa yanajidhihirisha kwa kutoka nje. Chochote unachobadili ndani huwa kinajionesha nje, hata unapokula chakula mwili wako unadhihirisha unakula chakula cha aina gani. Kila mtu anahitaji kufanya mabadiliko kwa sababu usipofanya mabdiliko utajiona wewe ni mzembe wakati wenzako wakibadilika.

Kwahiyo rafiki, nimekuandalia kitabu kizuri kwa ajili ya mabadiliko na kitabu chenyewe siyo kingine bali ni MABADILIKO 250 YA USHINDI. Kila mmoja anapigania kupata ushindi hivyo kupitia kitabu hiki cha Mabadiliko 250 Ya Ushindi kitakusaidia kufanya mabadiliko ya kweli katika maisha yako.

Mabadiliko ya kweli yatakupa mafanikio ya kweli, tunahitaji mabadiliko ya kweli katika maisha yetu ili tuwe na mafanikio ya kweli. Hivyo kitabu cha Mabadiliko 250 Ya Ushindi kipo tayari kwa ajili yako, napenda kukualika uweze kujipatia nakala yako leo.

Kitabu cha Mabadiliko 250 Ya Ushindi kipo katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy kinaweza kukufikia mahali popote pale ulipo. Ukiwa na simu janja, tablet, kompyuta basi unaweza kukisoma kitabu hiki na kufurahia maarifa mazuri yaliyoko ndani ya kitabu hiki.

Je kitabu hiki ni kwa ajili ya watu gani? kitabu hiki ni kwa ajili ya watu wote wanaohitaji mafanikio ya kweli katika maisha yao. Bila kufanya mabadiliko ya kweli, ndani huwezi kupata matokeo bora kwenye maisha yako.

Bei ya kitabu ni shilingi elfu kumi tu 10000/= lakini habari njema ni kwamba kuanzia leo tarahe  20 kitabu hiki kitaanza kuuzwa kawa bei ya ofa ya punguzo la bei badala ya shilingi shilingi elfu 10 utakipata kwa bei ya ofa ya shilingi elfu 5 hivyo kuwa wa kwanza kukisoma kitabu hiki kwa bei ya shilingi elfu tano. Ofa hii itadumu kwa kuanzia leo tarehe 20/3/2018 mpaka tarehe 25/3/2018 na baada ya hapo kitabu kitakuwa kinapatikana kwa shilingi elfu 10 baada ya ofa kuisha.

Je unahitaji mafanikio ya kweli? Kama ndiyo basi fanya mabadiliko ya kweli sasa kwa kutuma malipo ya shilingi elfu tano kwa bei ya ofa kwenda namba 0717101505 kwa tigo pesa au airtel money na 0767101504 kwa mpesa. Baada ya kutuma malipo tuma email yako au barua pepe yako kupitia namba ambayo umefanya nayo malipo na utatumiwa kitabu punde tu baada ya kutuma email yako.

Furahia mabadiliko ya kweli kwa sababu mabadiliko ya kweli huleta mafanikio ya kweli na kitabu cha Mabadiliko 250 Ya Ushindi kitazalisha mabadiliko mengi ndani yako kwa sababu kwenye kila badiliko moja utakalosoma litazaa mabadiliko mengine mengi.

Karibu sana rafiki tuendelee kujifunza kila siku,kama ukitumia maarifa vizuri unayopata hakika hayawezi kukuacha kama ulivyokuwa awali na hii ndiyo siri kubwa ya maarifa.

MUHIMU; Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la MIMI NI MSHINDI jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya HAPA. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya Kiswahili bonyeza Hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana P

%d bloggers like this: