Rasilimali yenye uhaba kwa kila mtu ni fedha. Kila mtu ana uhaba wa fedha hilo halina ubishi, ndiyo maana kila siku mtu anajituma ili kuendelea kupata fedha zaidi. Ingekuwa haina uhaba basi watu wasingefanya kazi kwa sababu inapatikana kirahisi. Angalia muda, ni rasilimali ambayo inaleta kila kitu kwenye maisha lakini haina uhaba watu wanatumia muda …
Mbinu Ya Kutokujiumiza Pale Unapopoteza Fedha
Pata picha inavyokuuma pale unapopoteza fedha, utajisikiaje? Kila mmoja wetu kuna maumivu ambayo anayapata pale anapopoteza fedha zake. Iko mbinu ambayo inaweza kukusaidia kutokuumia pale unapopoteza fedha. Ukipoteza fedha chukulia kama umetoa sadaka au umemmsaidia mtu asiyejiweza kwa kufanya hilo litakuzuia usiumizwe na kupotea kwa fedha. Bila kufanya hivyo, utajikuta unajiumiza kila wakati. Hatua ya …
Continue reading "Mbinu Ya Kutokujiumiza Pale Unapopoteza Fedha"
Msingi Wa Kupata Fedha Zaidi
Msingi ni huu; kila unapokuwa unahitaji fedha zaidi, jiulize swali hili, ni mtu gani naweza kumsaidia apate fedha zaidi? Ukipata jibu, hapo ndipo mahali unapoweza kupata fedha zaidi. Utaweza kupata fedha zaidi pale tu utakapomwezesha mtu mwingine kupata fedha zaidi. Makosa makubwa ambayo watu wengi huwa wanayafanya kwenye kutaka kupata fedha zaidi ni kuangalia ni …
Kabla Mteja Hajanunua Bidhaa au Huduma Unayouza Lazima Kwanza Anunue Kitu Hiki Kutoka Kwako
Huwa tunafikiri katika mauzo wateja wanaanza kununua bidhaa zetu, kitu ambacho siyo sahihi. Iko hivi rafiki yangu, kabla mteja hajanunua bidhaa au huduma Unayouza Lazima kwanza akununue wewe muuzaji. Ili mteja akununue wewe muuzaji lazima kwanza muuzaji uwe unauzika. Muuzaji ukiwa hauuziki watu watakuwa hawana mpango hata wa kununua kile unachouza. Unatakiwa uwashawishi watu kwa …
Usitafute Huruma Kwa Watu Wengine
Ni kawaida yetu sisi binadamu pale tunapopitia changamoto mbalimbali zinazotukabili huwa tunaona ni vema na haki kutafuta huruma kwa watu wengine juu ya yale tunayopitia. Tunafikiri kwamba, kwa njia ya kuwaelezea wengine matatizo yetu ili watuhurumie ndiyo tunaweza kutatua tatizo. Pambana na hali yako, usitafute huruma kwa watu, kila mtu ana changamoto zake hivyo yakabili …
Chukua Karatasi Yako Na Weka Sahihi Yako
Leo nataka kukuonesha ni kwa jinsi gani wewe uko tofauti na wengine na wakati mwingine nakushagaa pale unapotaka kuwa kama wengine badala ya kuwa kama wewe. Pata picha unachukua kalamu na karatasi yako halafu unaandika saini yako. Kisha angalia saini yako inafanana na ya mtu mwingine yeyote hapa duniani? Utajisikiaje kama hakuna mtu ambaye ana …
Hakuna Mtazamo Wa Hovyo Duniani Kama Huu
Kwenye kitabu chake jinsi ya kuuza chochote mwandishi Joe Girard anatuambia hakuna mtazamo wa hovyo duniani kama kuamini kwamba kitu hakiwezi kufanyika kwa sababu hakijawahi kufanywa. Mtazamo huo ndiyo umewafanya wengi kushindwa kupiga hatua, kwa kuendelea na mazoea. Hata kama hakuna mtu mwingine amewahi kufanya kitu fulani, kama umeona ndiyo unapaswa kukifanya ili kupata matokeo …
Asante Ya Mtu Huyu Inapaa Mbinguni
Huwa tunafikiri kutafuta ufalme wa Mungu ni kusali na kuhudhuria kwenye nyumba za ibada mara nyingi. Sina uhakika kama itakufaa lakini kutafuta ufalme wa Mungu ni pamoja na kusaidia watu wake. Hata yule anayesali sana hajawahi kumuona Mungu kwa macho, ni katika kusaidia watu wake ndiyo tunamuona Mungu kwa macho. Unaposaidia watu kupitia kile unachofanya, …
Jilazimishe Kuishiwa Kiakili Kwenye Eneo La Fedha
Kutoka kwenye kitabu cha Tano za Majuma Ya Mwaka, kilichoandikwa na Kocha Dr Makirita Amani, kuna dhana ambayo nilijifunza katika eneo la fedha, nimeona ni vema na wewe nikushirikishe. Karibu sana rafiki yangu, "Kilio cha wengi kwenye fedha ni kwamba, watu wakipata fedha haikai na hata wakiweka akiba, haikai. Yaani wakipata fedha au wakiwa na …
Continue reading "Jilazimishe Kuishiwa Kiakili Kwenye Eneo La Fedha"
Ukitaka Kuharibu Mahusiano Yako Kuwa Mtu Wa Hivi
Kuna baadhi ya changamoto kwenye mahusiano huwa tunazinunua sisi wenyewe kwa kujitakia. Sisi binadamu ni viumbe vya hisia, hivyo unapokuwa katika mahusiano na watu wengine jitahidi sana kuangalia hisia za watu. Watu wanafanya maamuzi yao kwa hisia, na siyo kwa fikra. Ukitaka kuharibu mahusiano yako na watu wengine kuwa mkosoaji. Hakuna mtu anayependa kukosolewa. Ukitaka …
Continue reading "Ukitaka Kuharibu Mahusiano Yako Kuwa Mtu Wa Hivi"