Design a site like this with WordPress.com
Get started

KITABU; JIPATIE NAKALA YA KITABU CHA IJUE NJAA YA WANANDOA

Mpendwa rafiki yangu,

Hongera sana kwa kazi na juhudi unazoendelea kuweka kuhakikisha unakuwa na maisha bora pamoja na kugusa maisha ya wengine.

Rafiki nina zaidi ya miaka mitatu sasa tokea nianze kuandika, kupitia mafundisho haya ninayoendelea kuyatoa yameweza kuwasaidia wengi na kugusa maisha yao kwa namna moja au nyingine.

Nimekuwa naandika eneo la mahusiano hivyo kupitia wale niliokuwa nawahudumia nimeweza kukutana na changamoto nyingi ambazo zote kwa pamoja zikanipelekea nikae chini na kuandika kitabu. Wengi waliniomba niandike kitabu kinachohusu mambo ya ndoa hivyo tokea mwaka jana mapema nikaanza kuandika kitabu hicho na hivi sasa kitabu hiko kipo tayari.

Rafiki, shabaha ya makala hii kwako ni kutaka kukujulisha kuwa nimetoa kazi nyingine mpya ambayo kazi hii imegusa eneo la mahusiano kwa ujumla. Kama tunavyojua tunaweza kufanikiwa katika maisha yetu lakini kama tumeshindwa kufaulu eneo la mahusiano basi mafaniko yetu yanakuwa hayana maana. Je ni nani kati yetu hayuko katika mahusiano? Kila binadamu asili yake ni mahusiano kadiri ya vinasaba yaani DNA.

Kazi ambayo nimefanikiwa kuandika ni kitabu cha kipekee sana kiitwacho IJUE NJAA YA WANANDOA.

Ijue Njaa Ya Wandoa, Kwanini Unavumilia Maisha Ya Ndoa Badala Ya Kufurahia?

Je unaijua njaa ya wanandoa? Kama jibu lako ni hapana basi kupitia kitabu hiki nimekuandalia mafundisho mazuri yatakayokusaidia eneo la mahusiano yako yaani ya ndoa, uchumba  na mahusino kwa ujumla.

Kitabu hiki kina sura kumi ambapo kila sura imesheheni maarifa sahihi ya kutuwezesha kuwa na furaha katika ndoa zetu. Wengi wamekuwa ni watu wa kuvumilia maisha ya ndoa lakini siyo kufurahia na kufurahia maisha ya ndoa ndiyo kusudi la ndoa yenyewe.

Kabla sijamaliza nikuache na moja ya maneno ya  kocha Dr. Makirita Amani baada ya kukisoma kitabu hiki na kuandika dibaji yake.  ‘’ kama upo kwenye ndoa au unapanga kuingia kwenye ndoa basi unapaswa kusoma kitabu hiki. Kama upo makini na maisha yako na unataka kuwa na mahusiano bora na watu wengine hakikisha unasoma kitabu hiki. Na kwa kuwa tunajua hakuna binadamu ambaye ni kisiwa, wote tunahusika na wengine, hivyo basi kusoma kitabu hiki ni moja ya hitaji muhimu la kuwa na maisha bora’’

Kwa namna ya pekee nimshukuru sana Makirita kwa ustadi wa hali juu kwa jinsi alivyoandika dibaji ya kitabu hiki, ili kuweza kujua njaa ya wanandoa na kujua kile alichoandika kocha Makirita katika dibaji yake iliyoko ndani ya kitabu hiki usipange kukikosa kukisoma kitabu hiki.

Je utaratibu wa kupata kitabu hiki ukoje?

Utaratibu wa kupata kitabu cha ijue njaa ya wanandoa ni kama ifuatavyo;

Kitabu kipo katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy. Kitabu hiki unaweza kukipata ukiwa sehemu yoyote duniani iliyo na mtandao wa intanenti. Kitabu hiki unaweza kusomea kwenye sehemu zifuatazo kwenye simu yako yaani smart phone au simu janja, kwenye pc au kompyuta yako na hata kwenye tablet yako. uzuri wa kitabu hiki unaweza kutembea nacho na kila unapopata muda unakaa chini na kusoma maarifa yaliyoko ndani yake.

Bei ya kitabu ni shilingi ngapi?

Bei ya kitabu ni shilingi elfu 10. Lakini kwa kuwa wewe ni rafiki yangu na ninakupenda sana nimeamua kukiuza kitabu hiki kwa bei ya ofa ambayo ni shilingi elfu tano.

Bei ya ofa ya kitabu hiki itakuwa ni shilingi elfu tano tu na ofa hii itakuwa ndani ya siku tatu tu, ambayo itaanza kuanzia tarehe 3 mpaka tarehe 5 ya mwezi Juni.

Je unapendwa kupitwa na ofa hii? Kama jipu lako ni hapana basi fanya malipo yako kupitia njia hizi. Tuma malipo kwenda Mpesa kwa namba 0767101504 na kwa wale wanaotumia Tigo pesa au Airtell Money tuma malipo kwenda namba 0717101505. Na uzuri wa mitandao ya siku hizi unaweza kutuma fedha kwenda namba ya mtandao wowote hata ukiwa na laini ya aina moja kama vile tigo, voda nk.

Kwahiyo, tunapaswa kufurahia ndoa zetu na siyo kuvumilia. Na kitabu hiki ndiyo majibu ya maswali yako kwanini watu wengi wanavumilia maisha ya ndoa badala ya kufurahia. Karibu usome kitabu hiki ili uijue njaa ya wanandoa.

Muhimu; kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la mimi ni mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa. Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga bofya hapa au nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili bonyeza hapa.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana

 

%d bloggers like this: