Design a site like this with WordPress.com
Get started

Namba Hazidanganyi

Ukiwauliza maswali watu kwamba wanaendeleaje? Watakujibu wanaendeleaje vizuri tu, wengine watasema Mungu anasaidia kwa kweli. Ukija katika upande wa namba majibu wanayotoa watu na namba haziendani kabisa kwa mfano, kwenye biashara, muulize mtu biashara yako inaendaje? Atakujibu inaendelea vizuri tu, Sasa ukitaka kumuuliza namba kwa mfano,mauzo yako yakoje?una wateja wangapi, wangapi ni wapya na wangapi …

Kama Unauchukia Umasikini Huwezi Kuwa Hivi

Umasikini siyo utakatifu wala utajiri siyo dhambi. Kama umasikini unakuumiza na unapenda kweli kubadilika kwenye maisha yako, huwezi kuwa na mjadala kwenye kazi. Kama unataka kufika mbali, huwezi kuwa na mjadala kwenye mambo yako muhimu kama vile uamke asubuhi na mapema ukafanye kazi au ulale. Huwezi kuwa na mjadala kwenye mambo muhimu, yaani ukipanga umepanga, …

Usiangalie Changamoto Unazopitia

Kwenye maisha hakuna eneo ambalo unaweza kwenda na unakuta hakuna changamoto. Au ulishawahi kuona nyumba gani iliyobandika bango mlango lenye ujumbe huu hapae. HAPA HAKUNA MATATIZO.?binafsi sijawahi kuliona hilo bango. Hii ina maana gani kwetu? Ina maana kwamba, hakuna sehemu ambayo ni salama hapa duniani. Kila sehemu ambayo unafikiria ukifanya kazi ndiyo utakutana na bango …

Huwezi Kukimbia Mchakato

Warren Buffett amewahi kusema huwezi kupata mtoto ndani ya mwezi mmoja kwa kuigawa mimba moja kwa wanawake 9. Mimba lazima ichukue miezi 9 kukamilika kuwa mtoto. Ili uweze kufanikiwa kwenye jambo lolote lile, unapaswa kukaa kwenye mchakato wa kile unachotaka. Usikimbilie matokeo kabla hujakaa kwenye mchakato. Kama tulivyooona kutoka kwa Warren Buffett, huwezi kurahisha kazi …

Watu Hawapati Fedha Kwa Sababu Hii

Watu wanatafuta hela ndiyo maana hawapati hela. Ukiwa ni mtu wa kutafuta hela, utapata shida kupata hela kwa sababu, ili upate hela unatakiwa utoe HUDUMA. Watu wengi hawatoi huduma ndiyo maana hawapati hela. Kwa mfano, mtu mwingine akiwa ameshapata hela haendelei tena kutoa huduma kwa sababu ana hela ya kula. Kwenye kutoa huduma bora ndiyo …

Nyota Njema Huonekana Asubuhi

Waswahili wanasema, nyota njema huonekana asubuhi, ni kweli nyota njema huonekana asubuhi.Lakini, kwenye maisha chochote kinaweza kutokea. Nyota njema inaweza isionekane asubuhi lakini ikaja kuonekana jioni. Kwenye biashara au maisha kwa ujumla muda wowote ule nyota njema huonekana. Inaweza kuwa asubuhi au jioni au wakati wowote.Unaweza ukakaa kwenye biashara siku nzima na usiuze, lakini kabla …

Watu Wote Wanaofanya Wanatumia Mbinu Hii Hapa

Kwenye maisha kuna vitu ambavyo havina mjadala na kuna vitu ambavyo vina mjadala ili vifanyike. Kwenda kujisaidia, kula, kulala, kupiga mswaki ni vitu ambavyo haviitaji mjadala ikishafika wakati wake unafanya tu, hujiulizi nikajisaidie au nisiende. Lakini sasa, INAPOKUJA kwenye vitu vya maana ambavyo vinatupa fedha kama kazi, biashara au hata kusoma vitabu na kujifunza kuwa …

Ukikosa Vitu Hivi Viwili Utanyanyasika Sana

Ukivikosa vitu hivi, siyo tu utanyanyasika lakini pia hutathaminikiwa. Ni asili kabisa na kamwe huwezi kwenda kinyume na asili. Vitu ambavyo kama huna basi utaishia kuburuzwa ni;Moja, huna fedha. Fedha ni jawabu la mambo yote. Sehemu yoyote ile ukikosa fedha utadharauliwa. Tukiachana na hewa tunayovuta, kinachofuata kwa umuhimu ni fedha. Fedha ndiyo inaendesha maisha yetu, …

Ukitaka Kujua Kama Unaenda Mbele Au Unarudi Nyuma Kifedha

Maisha ni namba.Chochote ambacho hakipimwi hakikui. Na maisha ambayo hayatathiminiwi ni maisha ambayo hayana maana kuishi. Ni kazi kujua kama unaenda mbele au unarudi nyuma kifedha kama hujipimi. Ili uweze kujua kama unaenda mbele au unarudi nyuma kifedha unatakiwa kujipima kinamna hii. Moja andika kila fedha unayopata kila siku, halafu mwisho wa siku, wiki na …