Design a site like this with WordPress.com
Get started

Mahusiano Mazuri Ni Maisha Mazuri

Iko hivi rafiki yangu, Mahusiano mazuri ni maisha mazuri na mahusiano mabaya ni maisha mabaya. Hakuna mafanikio yanayopatikana katika mahusiano mabaya, ukitaka kuwa na mafanikio unapaswa kuwa na mahusiano mazuri na wale unaojijusisha nao.Mahusiano mabaya yanaumiza, yanakufanya ushindwe kufokasi katika kazi. Muda mwingi utautumia katika kusuluhisha migogoro badala ya kufanya kazi. Weka juhudi kwenye kujenga …

Utakuja Kumwitaji Tena Baadaye

Milima huwa haikutani ila binadamu tunakutana, wahenga walisema hivyo. Jamii yetu imekuwa na mtazamo wa hovyo na wa tofauti sana. Mtu anapokuwa anahusiana na mtu mambo yanakuwa mazuri lakini wakishindwa kuelewana kwenye kitu kidogo tu, basi kisirani kinaanzia hapo. Sina uhakika kama itakufaa lakini kama umeachana na msaidizi wako kwenye biashara, nyumbani, mpenzi au mchumba …

Sala Dhidi Ya Kuwasema Wengine Vibaya

Usiwaongelee  wengine  vibaya, najua kuna watu wengine hawawezi kumaliza siku bila kuwasema WENGINE vibaya. Midomo yao iko kama vile bata ambaye hawezi kujizuia pale anapotaka kujisaidia. Nakusihi sana acha kusema watu vibaya, wewe siyo kiranja wa dunia ambaye unataka watu wawe kama vile unavyotaka wewe. Ukikosa mazuri kwa mtu ya kusema, basi kaa kimya na …

Ukitaka Kuoa Au Kuolewa Olewa Au Oa Mtu Huyu

Kwanza kabisa nikuambie tu kitu rafiki yangu nikupendaye, Huwezi kubadilisha asili ya mtu hata siku moja. Kama ulioa au kuolewa ukiwa na lengo la kutaka kumbadilisha mtu awe kama unavyotaka wewe hapo umejidanganya. Ukweli ni kwamba, ukitaka kuoa au kuolewa, oa au olewa na mtu ambaye hutaki kumbadilisha. Matatizo mengi kwenye mahusiano huwa yanayokea pale …

Umuhimu Mkubwa Wa Kuimarisha Mahusiano Yako

Iko hivi rafiki yangu nikupendaye, Kwa chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, utakipata kwa watu wengine. Mafanikio unayotaka kuyaona kwenye maisha yako, watakaokusaidia kupata ni watu wengine. Kifupi kile tunachotaka tutakipata kupitia watu wengine, watu wanakutegemea ili wafanikiwe kupitia wewe. Unahitaji  kuwa  na  mtandao  wa  watu  ambao  wanaweza  kukusaidia  kwenye  maeneo mbalimbali  na  wewe  pia  …

Epuka Tabia Hii Kwenye Mahusiano Yako

Kiasili kila binadamu anapenda kusifiwa. Kila binadamu anapenda kuonekana anathaminiwa. Kitu ambacho kinavuruga mahusiano yetu na wale tunaohusiana nao ni kukosoa. Kwa mtu yeyote yule unayehusiana naye, ukitaka kuboresha mahusiano yenu, iwe ni ya kazi, biashara, ndoa na nk msifie na usimkosoe. Wapende na wachukulie watu kama walivyo. Tafadhali kazi yako isiwe ya kukosoa bali …

Jinsi Ya Kuwapenda Watu

Njia bora ya kuwapenda watu na kujenga mahusiano bora ni kuwakubali watu kama walivyo. Bila ya kutaka wabadilike au wawe kama unavyotaka wewe. Lakini, ukishaanza kusema unawapenda watu kwa sababu wako kwa aina fulani na ukishaanza kutaka watu wabadilike na kuwa kama unavyotaka wewe ndiyo uwapende, jua hapo hujawapenda watu. Kamwe haitatokea kila mtu kwenye …

Kitu Ambacho Wanandoa Wengi Hawana

Wengi wanaishi kwenye ndoa lakini afya yao ya ndoa siyo nzuri. Hivi nikiuliza vipi afya yako ya ndoa ndani ya miaka 10 au mitano iliyopita utasemaje? Ndoa ni biashara kama zilivyo biashara nyingine kwa sababu kwenye biashara, ikiwa biashara haina mzunguko mzuri yaani afya yake haiko vizuri ni rahisi kuanguka. Kuna vitu vidogo vidogo tu …

Kabla Hujampenda Mtu Yeyote Mpende Kwanza Huyu

Jipende kwanza wewe mwenyewe. Mtu anayefanya vizuri kwenye eneo lolote lile ni yule ambaye anaanza kujipenda yeye mwenyewe kwanza. Unapojipenda wewe mwenyewe kwanza, itakulazimisha hata wale waliokuzunguka wawe bora na wajipende wao wenyewe. Kwa sababu, hatuwezi kuwabadilisha watu wawe vile tunavyotaka sisi pasipo sisi kuwaonesha kwa vitendo. Hatuwezi kuwapenda wengine kama sisi wenyewe hatujipendi. Falsafa …

Ukitaka Kuharibu Mahusiano Yako Kuwa Mtu Wa Hivi

Kuna baadhi ya changamoto kwenye mahusiano huwa tunazinunua sisi wenyewe kwa kujitakia. Sisi binadamu ni viumbe vya hisia, hivyo unapokuwa katika mahusiano na watu wengine jitahidi sana kuangalia hisia za watu. Watu wanafanya maamuzi yao kwa hisia, na siyo kwa fikra. Ukitaka kuharibu mahusiano yako na watu wengine kuwa mkosoaji. Hakuna mtu anayependa kukosolewa. Ukitaka …