Design a site like this with WordPress.com
Get started

Soma; Simulizi Nzuri Ya Kusisimua Yenye Mafundisho Mazuri Ndani Yake

Habari za leo mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Naamini mu wazima afya na mnaendelea vizuri katika kusukuma gurudumu hili la maisha. Karibu sana rafiki na katika makala yetu ya leo nitakushirikisha simulizi nzuri yeye mafundisho kwenye maisha yetu. Nakusihi tusafiri pamoja ili uweze kujifunza mazuri kupitia hadithi hii.

Image result for fisher in the river

Kulikua na baba mmoja aliyekua anafanya kazi ya kuokoa watu waliokuwa wanatumbukia katika maji kwa ajali ya mitumbwi pindi walipokuwa wanavuka ng’ambo moja kuelekea ng’ambo nyingine. Baba huyu pia alikuwa mvuvi wa samaki akishirikiana na wafanyakazi wenzake katika kazi hiyo ya uvuvi. Baba huyu alikua anaokoa watu mbalimbali na baada ya kuokoa watu hao hakuna hata mtu mmoja aliyerudi nyuma kumshukuru. Kila mtu alienda kutoa shukrani kanisani.

Kitendo cha kwenda kutoa shukrani kanisani kilimuumiza sana, alitaka aje apewe shukrani yeye mwenyewe hata kwa kumletea pea moja ya viatu au nguo za kuvaa. Baba Yule alikata tamaa kabisa na kusema kuwa haitakuja kutokea hata mara moja kuja kuokoa tu aliyezama baharini kutokana na ghadhabu aliyoipata kutokana na watu aliokwisha kuwaokoa kutorudi kumshukuru hata kwa zawadi.

SOMA; Mambo Muhimu Niliyojifunza Katika Kitabu Cha The Total Money Makeover

Siku moja mke wake alimuomba kwenda kusalimia wazazi wake kijiji cha jirani . Mume huyo alikubali na akamruhusu aende na watoto na warudi nyumbani baada ya wiki moja.Mama Yule alipofika nyumbani kwao hakumkuta mtu yeyote kwani wazazi wake walikuwa hawapo. Mke wa baba Yule akaamua afunge safari tena kurudi nyumbani kwake akiwa ameambatana na watoto wake wawili. Mama na watoto wake wawili waliamua kupanda mtumbwi uliokuwa pembezoni mwa bahari tayari kwa kurudi nyumbani.

Walipokuwa mtumbwini na katikati ya bahari dhoruba kali ikaja ikawakumba nawakazama maji. Muokoaji wa wazama maji ambae ndie aliyekuwa mume wake akaitwa haraka na watu kuwa kuna mtumbwi umezama hivyo akasaidie kuokoa watu waliozama baharini. Baba Yule alikataa katukatu kwenda kuokoa na kusema haendi kuokoa mtu yeyote kwani hawamlipi kitu chochote baada ya uokozi.

Watu wale walizama baharini na baadaye kuelea juu ya maji ndipo watu walipoenda kuwachukuwa wakiwa wameshakufa maji. Watu hao walikuwa ni mama ambae ni mke wake pamoja na watoto wao wawili. Watu walioenda kuwachukua wafa maji wale walishtuka sana walipoona ni mke na watoto wa baba Yule. Walienda kumwambia twende ukaone mke wako na watoto wamekufa maji, baba Yule alikataa na kusema hapana sio mke na watoto wangu kwani mke na watoto wangu watarudi wiki ijayo.

SOMA; Haya Ndio Mambo Manne (04) Yanayokwenda Kinyume na Falsafa Ya Upendo Hapa Duniani

Watu wale walimsihi baba Yule na kwa pamoja wakaenda na walipofika pale baba Yule alishtuka sana kukuta ni mke na watoto wake ndio wamekufa maji. Alilia kwa uchungu mkubwaambao hauelezeki. Basi walibeba maiti zile na kuelekea nazo kijijini kwao kwa ajili ya maziko. Baba Yule alilia sana kwa pigo lile kwani siku aliyogoma kuokoa wazama maji ndio siku hiyohiyo mke wake na watoto walipozama maji bila msaada wowote. Aliishi kwa uchungu mkubwa maisha yake yote na mwisho wa mke na watoto wake uliishia pale sababu ya kiburi cha baba Yule kukataa kusaidia watu.

Rafiki, tunapata mafunzo gani kupitia hii hadithi? Yafuatayo ni mafunzo niliyopata kupitia hadithi hii.
1. Tenda wema uende zako na usingoje shukrani , kama umepanga kusaidia watu saidia na wala usingoje shukrani kwani huwajawahi kusikia shukrani ya punda ni mateke? Utawasaidia wengi katika maisha yako lakini siyo wote watarudi kutoa shukrani.

2. Fanya kazi kwa moyo, kama umechagua maisha kujitoa na kusaidia watu basi jitoe kwa moyo bila manung’uniko yoyote yale. Usiangalie malipo na kuwa hela mbele kuliko utu. Saidia watu kwa kile Mungu alichokujalia kama wewe ni mwalimu wafundishe watu, kama wewe ni mwanamziki imba nyimbo nzuri za kuelimisha na kuburudisha watu hata kama watu hawakupi shukrani. Wewe kama ni mwandishi andika watu wajifunze kile unachojua kwa kufanya hivi utakua umeikomboa dunia.

3. Mambo hayawi kama unavyodhania, tunaona katika simulizi yetu nzuri ya hadithi huyu mvuvi alikuwa anaambiwa kuwa kuna watu unatakiwa ukawaokoe wamezama yeye akapuuzia na kujifariji kuwa mke wake alifika salama kule aendako kumbe mambo yalikuwa ndivyo sivyo. Usitegemee mambo yatakuwa kama vile ulivyopanga wewe hivyo jiweke tayari kupokea chochote kwani nyakati ngumu hazina hodi katika maisha yetu.
Hatua ya kuchukua leo, andika mambo yote ulijifunza katika simulizi hii na fanyia kazi yale muhimu ulijifunza. Unaweza pia ukanishirikisha yale uliyojifunza kupitia barua pepe yangu kama ukipenda.

Mwisho, kila mmoja wetu ana umuhimu wake hapa duniani. Kila mmoja wetu ana kitu cha kikee hapa duniani cha kuweza kuifanya dunia kuwa bora. Kila mmoja wetu ana mchango wake hapa duniani. Je wewe mchango wako nini hapa duniani? Hivyo tumia talanta yako kuing’arisha dunia.

Kama ulikuwa bado hujajiunga na mfumo wetu wa kupokea makala kwa njia ya email list jiunge leo ili uweze kupokea vitabu mbalimbali na makala mbalimbali. Pili, kama ulikuwa bado hujalaiki ukurasa wetu wa facebook fanya hivyo leo rafiki. Pia kama ulikuwa bado hujasoma kitabu kizuri cha funga ndoa na utajiri wahi mapema kujipatia nakala yako ambayo iko katika mfumo wa nakala tete yaani soft copy tuwasiliane kwa namba hii 0717101505/0767101504 kupata kitabu hiko. Mwisho, usisahu pia kumshirikisha na mwenzako makala hii nzuri uliyosoma leo. Hakikisha na mwenzako anapata maarifa haya mazuri.

Nakutakia kila la heri katika haya uliyojifunza leo. Endelea kutembelea mtandao huu kujifunza kila siku. Asante sana.
Rafiki na mwalimu wako,
Deogratius Kessy
0717101505 /0767101504 au deokessy.dk@gmail.com

Published by Deogratius Kessy

Mwandishi,mwalimu na mjasiriamali. Unaweza kutembelea Blog yake ya www.kessydeo.home.blog kujifunza zaidi na unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: