Usiogope Kuuliza Kitu Hiki Kwenye Maisha Yako

Kuuliza siyo ujinga. Unapokuwa una safari kwenda sehemu usiyojua yaani wewe unakuwa mgeni huwezi kuona aibu wala kuogopa kuuliza.Lazima utauliza ili usije ukapotea lakini pia uweze kufika kule unakotaka kufika. Unapokuwa hujui kitu, usiogope kuuliza kitu. Hakuna mtu anayejua kila kitu, hivyo unapomuuliza mtu atakujibu kama kipo ndani ya uwezo wake.Na mara nyingi watu wanapenda [...]

Usimchinje Ng’ombe Wako Kwa Oda Ya Maini

Ni watu wa chache sana wanaishi maisha wanayotaka kwa sababu wengi hawaishi vile wanavyotaka bali wanaishi vile wanavyotaka wengine. Je hayo maisha unayoishi ndiyo maisha yako halisi? Huwa tunaigiza maisha yetu mchana lakini ikifika usiku huwa tunakutana na sisi wenyewe tunajiona kabisa ni watupu na kile tunachofanya siyo sahihi. Utaweza kuwadanganya watu wote lakini huwezi [...]

Hii ndiyo Njia rahisi kuliko zote duniani za kuwa tajiri

Wote tunajua kuwa ni jinsi gani fedha ilivyokuwa muhimu kwenye maisha yetu. Inatusaidia kuendesha maisha yetu na kulipa bili mbalimbali. Fedha ni muhimu kweli na hilo halina ubishi hata kidogo. Kila mtu anatamani awe na uhuru wa kifedha wa kumwezesha kufanya kile anachotaka na watu wengi hawana uhuru wa kifedha na dalili moja wapo ya [...]

Hiki Ndicho Unachotakiwa Kujali

Kuna mtu akiangalia historia yake ya maisha ilivyo anaweza kusema kuwa yeye hawezi kufanya kitu kadiri ya historia yake. Tunayo mifano ya watu wengi tu tokea enzi na enzi ambao walikuwa na historia mbaya lakini Mungu alikuja kuwabadilisha na kuwa watu wa historia nzuri. Ndiyo maana leo ninakuambia rafiki yangu, haijalishi unatokea wapi?, Kinachojali ni [...]

Mambo Mawili Unayopaswa Kuwa Nayo Ili Kutenda Miujiza Kwenye Maisha Yako

Kila mmoja wetu amezaliwa na uwezo mkubwa sana ndani yake lakini kadiri ya mazingira tunayoishi, mitazamo hasi tunayoingiza akilini inasababisha kushindwa kutumia uwezo mkubwa wa akili tulio nao. Wewe ni kiumbe uliyependelewa kuliko viumbe vilivyoko duniani lakini cha ajabu yake hutumii vema upendeleo huo ambao umejaliwa kuwa nao. Hivi ukijiuliza tunakwama wapi mpaka tunashindwa kufanya [...]

Unachokihofia Huwa Hakipo

Huwa tunatengeneza mazingira ya hofu ambayo hata haipo katika hali ya kawaida. Unakuta mtu anatengeneza mazingira ya hofu kiasi kwamba inamletea hata kushuka kwa ufanisi wake wa kazi. Pengine unajua siku fulani utakuwa na tukio fulani basi mtu anatengeneza mazingira ya hofu, anaanza kuiwazia hiyo siku itakuwaje na matokeo yake anaanza kujawa na hofu ambayo [...]

Kama Tatizo Lako Linatatuliwa Na Fedha Basi Jua Tatizo Lako Ni Hili Hapa

Ukichunguza matatizo mengi tuliyonayo chanzo kimoja ni fedha. Hata matatizo mengi uliyonayo siyo kwamba ni matatizo makubwa sana bali kuna kitu kinachangia wewe kuwa hivyo.Kumbe basi, matatizo mengi watu waliyonayo yanasabishwa na ukosefu wa fedha. Kama una matatizo, halafu tatizo lako linaweza kutatuliwa na fedha basi wewe huna tatizo hapo, Bali tatizo lako ni fedha [...]

Haya Ndiyo Mambo Mawili Yanayoweza Kutokea Katika Maisha Yako

Heri ya mwezi agasti, Unapopata muda wa kujitathimini katika kile unachofanya kila siku mambo hayawezi kwenda kama vile ulivyopanga au vile unavyotaka wewe. Hivyo basi, katika maisha yetu pale mambo yanapokwenda ndivyo sivyo hata usijilaumu sana bali pokea na shukuru jifunze kwa kile kilichotokea. Wakati mwingine huwa tunajiaandaa na ushindi ,tunapanga mambo yetu kama vile [...]

Create your website at WordPress.com
Get started