Kwenye maisha yako unapaswa kuwa mtu imara. Usipokuwa imara utawaruhusu watu wengine wakutawale na huwezi kuwa huru kwenye maisha yako kama umetawaliwa na mtu fulani.
Kwenye maisha yako usiwe mnyonge kabisa, jiamini, na simamia kile unachokiamini.
Kama unaishi bila kuvunja sheria za asili, nchi na kanuni za maadili huna cha kuhofia. Bali ishi kwa uhuru na kujiamini.
Maana ukitaka kuishi muda mrefu, kuwa mwangalifu kwenye kila eneo la maisha yako.
Usikubali anayekuonea aendelee na uonevu wake.
Usikubali kuwa mtu wa kuonewa na watu kukuchukulia ni kitu cha kawaida.
Simamia utu wako na yeyote anayekuonea mfanye ajifunze kwamba uonevu siyo kitu sahihi.
Sehemu yoyote jitetee kama mtu anataka akuonee pale ambapo wewe unaona kabisa ni uonevu.
Ni kawaida ya binadamu kuonea kile ambacho kipo dhaifu, usikubali kuwa dhaifu kuwa imara, fanya mambo yako kwa kujiamini, tembea mabega yakiwa nyuma.
Wewe ni mshindi na umezaliwa kushinda, hivyo mafanikio ni haki yako ya kuzaliwa usikubali kuwa mtu wa kuonewa hovyo.
Wewe ndiyo unaruhusu watu wa nje wakuonee kwa jinsi unavyoishi na unavyofanua mambo yako.
Anayekuonea muonesha kwako kuna moto na akijaribu unamuunguza. Kama kitu hukipendi kibadili na mwambie ukweli yule anayekukwaza usiendelee kumbeba mtu ambaye anakufanya uyachukie maisha yako.
Hatua ya kuchukua leo; usikubali anayekuonea aendelee na uonevu wake.
Usikubali kuwa mtu wa kuonewa na watu kuchukulia ni kitu cha kawaida, simami utu wako na yeyote anayekuonea mfanye ajifunze kwamba uonevu siyo kitu sahihi.
Usipopanga kuonewa na watu watakuonea, usikubali kuonewa, simama imara.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog