Design a site like this with WordPress.com
Get started

Vitu Viwili Muhimu Vya Kuzingatia Kwa Kila Muuzaji

Ni imani yangu kwamba kama uko hai, basi kuna kitu unaendelea kuuza hapa duniani.

Kwa sababu hakuna mtu ambaye anaweza kuendesha maisha yake pasipo mauzo.

Tunapouza maana yake tunatoa, na katika maisha asiyetoa maana yake hapokei, hivyo basi, kila anayetoa huwa anapokea kadiri ya sheria ya asili.

Ukiwa kama muuzaji bora kuwahi kutokea kwenye eneo lako, zingatia haya mawili.

Muuzaji bora anatakiwa kuzingatia mambo haya mawili;

Moja bidhaa bora. Bidhaa bora ndiyo injini ya mauzo, ukiwa na bidha bora ni rahisi sana kuuza.

Unatakiwa kuwa mwaminifu sana kwa bidhaa unayouza, unaposema bidhaa ni bora basi iwe bora kweli na inapotokea changamoto yoyote ile kwenye bidhaa baada ya kumuuzia mteja, unapaswa kuwajibika.

Wauzaji wengi wanakosea, lengo lao ni kuuza lakini wanafanya makosa ya kutowafuatilia wateja wao kwa bidhaa walizowauzia.

Usidanganye watu ili uuze, uza kitu ambacho hata mtu akinunua kinaenda kumsaidia kweli mteja na siyo kumuongezea matatizo zaidi.

Kitu cha pili ni huduma bora. Haitoshi kuwa na bidhaa bora, bali unapaswa kuwa navyo vyote viwili, bidhaa bora na huduma bora.

Watu wengi wana bidhaa bora lakini hawana huduma bora. Kitakachokufanya wewe uendelee kuuza ni kuwa na huduma bora wakati wote.

Huduma bora ndiyo tunapaswa kuona kwa wateja.
Kwa mfano, mtu x ana bidhaa bora lakini huduma yake ni mbovu, na mtu y ana huduma bora na bidhaa bora unafikiri kwa mtu mwenye akili timamu atahangaika kumpelekea hela mtu ambaye hajali?

Huduma yoyote unayotoa tafadhali toa kwa uaminifu mkubwa. Usidanganye ili upate fedha, toa thamani kubwa, tena itoe kwa upendo, ona kama vile mtu asipopata huduma yako basi kuna kitu anakosa, na jitahidi sana kumshawishi mteja mpaka umsaidie.

Hakikisha mazingira ya utoaji wa huduma yanakuwa bora.

Sikiliza wateja wako, kwani ndiyo mabosi wa biashara yako.

Jali maslahi ya wateja wako kwanza na yako yatafuata.

Kumbuka bidhaa ziko nyingi je, umejiandaaje kujitofautisha na wengine?

Hatua ya kuchukua leo; Toa huduma bora na zalisha bidhaa bora. Kwa kuzingatia vitu hivyo viwili fedha haiwezi kukupiga chenga kwenye biashara yako.

Kinachofuata baada ya hapo, hakikisha unafanya kazi kubwa ya masoko yaani ifanye biashara yako ijulikane na watu wengine, kuongeza wateja na kukazana kukuza mauzo yako na unayakuza kwa kujipa namba za kufanyia kazi kila siku, labda kwa wiki mauzo yako yawe kiasi fulani na kwa siku yawe kiasi gani halafu sasa unajisukuma kuhakikisha unafikia namba kwa kuuza kama vile chizi.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: