Hakuna kitu kipya mpaka sasa,mara nyingi mambo ni yaleyale lakini kwa nini inakuwa vigumu watu kuchukua hatua au kufanikiwa kwenye jambo fulani? Unafikiri ni kwa nini watu wanakuwa vilevile kila mara? Ni kwa sababu watu wanakosa uwajibikaji. Ni rahisi mwasibu aliyeajiriwa kufanya kazi vizuri alipoajiriwa ila ukija kwenye maisha yake binafsi hata mipango binafsi wala …
Category Archives: MAKALA ZA HAMASA
Nidhamu Ambayo Wengi Hawana
Ni nidhamu binafsi ya kujifuatilia. Ni rahisi mtu kufuatilia jinsi dunia inavyoenda kwenye mitandao ya kijamii, vyombo vya habari nk lakini wanajisahau kujifuatilia wao wenyewe. Kujifuatilia ni kazi, inahitaji nidhamu kali na wengi hawana, mtu anaweza kufuatilia Mambo ya wengine wakati hata kwake mwenyewe ameshindwa hata kufuatilia maendeleo ya watoto wake. Fuatilia namba muhimu kwenye …
Usirudie Tena Ujinga Huu
Ujinga Ni Nini ? Ujinga ni kurudia kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule halafu unategemea kupata matokeo tofauti. Kwa mfano, mwaka 2022 ulikuwa unafanya kazi au biashara kimazoea halafu mwanzoni mwa mwaka 2023 unajiambia mwaka huu lazima utafanikiwa. Utafanikiwa kwa namna gani kama mwendo uliotembelea mwaka jana unataka utembee nao mwaka huu? Lazima …
Hii Ndiyo Hamu Unayopaswa Kuwa Nayo Ili Kufikia Mafanikio Makubwa
Je, una hamu kiasi gani ya kufikia ndoto yako? Hamu kubwa unayokuwa nayo kwenye kitu unachotaka ndio inapima kama utaweza kukipata. Kama una hamu kubwa sana ya kupata kitu, hakuna kitu kitakachoweza kukuzuia kukipata. Hata utapokutana na changamoto lazima utapata njia. Hamu kubwa ya kupata kitu inakupa nguvu ya kulipa gharama ya mafanikio. Unaweza kujitengenezea …
Continue reading “Hii Ndiyo Hamu Unayopaswa Kuwa Nayo Ili Kufikia Mafanikio Makubwa”
Acha Kufanya Mambo Yasiyokuwa Sahihi
Ili uweze kwenda mbele, lazima kwanza uache kufanya mambo yasiyokuwa sahihi. Ukiwa ni mtu wa kufanya kazi na kufanyia kazi yale mambo sahihi tu lazima utafanikiwa. Hufanikiwi, kwa sababu unafanya mambo yasiyokuwa sahihi mengi. Ukifanya mambo sahihi, lazima utapata majibu sahihi. Mambo sahihi yanafanya kazi kama ukiyafanyia kazi. Ukiamua tu kufanya mambo sahihi lazima utapata …
Usiwe Na Wasiwasi Na Mtu Huyu
Usiwe na wasiwasi na nafsi yako mwenyewe. Kinachowazuia wengi kufanikiwa ni kuwa na wasiwasi juu ya nafsi zao wenyewe. Na ukishakuwa na wasiwasi huwezi kufanikiwa kwenye maisha yako. Kwa sababu adui mkubwa wa imani ni mashaka. Watu wana wasiwasi juu ya nafsi zao wenyewe kwa sababu walijaribu na kushindwa huko nyuma. Hivyo wanahofia kujaribu tena …
Kama Unataka Matokeo, Fanya Kitu Hiki
Rafiki yangu nikupendaye, Kinachokukwamisha na kushindwa kupata matokeo unayotaka ni kwa sababu moja tu nayo ni sababu unazojipa. Kuna sababu nzuri unazojipa ambazo zinakufanya usichukue hatua. Pale unapokutana na changamoto mbalimbali unajipa sababu ambazo ambazo unaona ni za kweli na zinakufariji. Nikuambie kitu, sababu unazojipa hazitokusaidia kulipa bili wala kubadilisha maisha yako. Na kitakachokusaidia kupata …
Mbinu Nzuri Ya Kutumia Pale Unapoona Umetingwa Na Mambo Mengi
Ukiona umebanwa na una mambo mengi ya kufanya huku muda wako ukiwa mchache unapaswa kufanya yafuatayo; Moja, futa yale yote yasiyo na tija kwako. Watu wengi wanasema wako bize lakini kwenye mambo ambayo hayana tija kwao. Jiulize, hicho kinachokufanya uwe bize kinaleta fedha mfukoni? Kama jibu ni ndiyo, endelea kukifanya lakini kama jibu ni hapana, …
Continue reading “Mbinu Nzuri Ya Kutumia Pale Unapoona Umetingwa Na Mambo Mengi”
Hujisukumi Kwa Sababu Huna Kitu Hiki
Kwa sababu huna kitu kinachokusukuma kufanya. Watu wengi wanaondoa uvivu, uzembe kama kuna kitu kinawasukuma ndani yao kufanya. Kama huna sababu inayokusukuma ya nini kujitesa? Ila ukiwa na sababu unakuwa unajisukuma kweli na huoni tena mateso bali unaona mateso ndiyo njia ya kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Mtu mmoja alikuwa na hali mbaya sana …
Usisubiri Mpaka Uwe Tayari
Ukisubiri mpaka kila kitu kiwe vizuri ndiyo uanze, kuna vitu unaweza kupata lakini ni vile vilivyoachwa na wale walioanza kabla ya hata ya kuwa tayari. Kama umeiona fursa ya biashara lakini hujaanza kwa sababu hujawa tayari, utakapokuwa tayari kuanza utapata wateja lakini ni wale ambao waliachwa na wale ambao waliweza kuanza kabla hata hawajawa tayari. …