Design a site like this with WordPress.com
Get started

KITABU; JIPATIE NAKALA YA KITABU CHA KWANINI MSAMAHA (WHY FORGIVENESS)

Habari mpendwa rafiki na msomaji wa mtandao wa Kessy Deo? Ni matumaini yangu kuwa hujambo na unaendelea vizuri.  Karibu sana rafiki tuweze kujifunza wote kwa pamoja.

Changamoto kubwa inayoyawaumiza watu wengi kushindwa kufurahia maisha ni maumivu ya nafasi. Kwa kwe,li watu wengi wamejeruhiwa, nafsi nyingi zimeumizwa, nafsi nyingi zina majeraha ya moyo, nafsi nyingi zina maumivu, nafsi nyingi zimebeba mizigo. Changamoto nyingine inayowatawala watu katika jamii yetu ni wivu na chuki inayopelekea watu kuishi maisha ambayo hayana maana wala thamani hapa duniani.

Displaying cover front.jpg

Familia nyingi si salama, ndoa nyingi, si salama, mahusiano mengi si salama hii ni kuanzia mahusiano ya kiujirani, ndugu, jamaa na hata marafiki na nk. Baada ya kuona na kufanya tafiti katika jamii nikagundua kuwa nafsi nyingi za watu zinasumbuliwa na majeraha mbalimbali ya moyo, maumivu ya ndani, wivu, chuki na uchungu uliombika ndani ya moyo. Hivyo basi, kwa kuwa nafsi nyingi za watu zina matatizo hivyo ninakaona ni vema na haki kuandaa kitabu kitakachokwenda kutibu nafsi za watu wengi.

Ndugu msomaji, ndipo niliposukumwa kuandika kitabu cha kwanini msamaha kwa msaada wa Mungu na hatimaye kukimalisha kuandika kitabu hiki. Kitabu cha KWANINI MSAMAHA yaani WHY FORGIVENESS ni kitabu maalumu kwa ajili ya kila mtu aliye na majeraha ya nafsi  au maumivu ya moyo na kushindwa kufurahia maisha.  Hivyo kitabu hiki kinakweda kutibu mioyo ya watu iliyokuwa imekufa na kuwa hai kupitia msamaha wa kweli kila mtu atakwenda kupata uponyaji wa nafsi kupitia msamaha wa kweli.

Rafiki, tunaalikwa kusamehe saba mara sabini hii ina maana kwamba kama wewe ni binadamu basi, unaalikwa kusamehe kila siku ya maisha yako. Bila msamaha basi maisha ya binadamu yatazidi kuwa machungu  na nafsi nyingi  Zitaendelea kuteseka lakini mwenyezi Mungu ambaye yeye ndiye mwasisi wa msamaha anatualika kuweza kusameheana kila siku ili nasi tuweze kusamehewa. Tunaalikwa kusamehe ili maisha yaende, ili mambo mengine yaende na tusamehe kwa faida yetu sisi wenyewe. Kupitia msamaha wa kweli utakwenda kurudisha uhusiano wako wa awali ambao ulikuwa umevunjika.

Kwahiyo, kwanini kitabu hiki cha KWANINI MSAMAHA? Kupitia kitabu hiki cha kwanini msamaha kina sura kumi na saba ambapo kila sura kuanzia sura ya kwanza mpAka ya mwisho kinakupa mafundisho muhimu juu ya msamaha.  Kwa mfano, sura ya kwanza utajifunza yafuatayo;

  • Msamaha ni nini
  • Sura ya pili, utajifunza aina za msamaha
  • Sura ya tatu utajifunza mambo mawili muhimu ya kuzingatia katika msamaha wa kweli
  • Sura ya nne utajifunza kwanini Kusamehe siyo kuvumilia au kusahau?
  • Sura ya kumi na mbili utajifunza chanzo kikuu cha maumivu ya ndani tunayopitia kwenye maisha yetu.
  • Kumi na tatu utajifunza chanzo kikuu cha wivu, matokeo yake na jinsi ya kuepuka.

Hizi ni baadhi tu ya sura ambazo nimekushirikisha vionjo vyake hapa na utakapojipatia nakala yako utajifunza yote muhimu kupitia kitabu hiki cha kwanini msamaha.

Jinsi ya kukipata kitabu hiki;

Kitabu hiki cha Kwanini Msamaha  kimeandikwa kwa lugha nzuri na rahisi ya Kiswahili, hivyo basi kitakuwa kinapatikana kwa mfumo wa nakala tete yaani soft copy na baadaye kitapatikana katika mfumo wa hard copy. Kitabu hiki kitakufikia popote pale ulipo duniani na utaweza kukisoma kitabu hiki kupitia simu yako ya mkononi, tablet na hata kompyuta.

Kitabu hiki kitapatikana kwa bei ya shilingi elfu tano, na utatumiwa kwa njia ya barua pepe yaani email yako, kama huna email hakikisha una email, au kwa njia ya wasapu na telegram utaweza kutumiwa kitabu hiki na kukufikia hapo ulipo.

Ndugu msomaji, kuhakikisha hukosi nakala yako ya kitabu hiki cha kwanini msamaha unaalikwa kutuma pesa ya shilingi elfu tano (5000) kwa njia ya mpesa 0767101504, na tigo pesa au airtel money 0717101505. Baada ya kutuma malipo hakikisha unatuma ujumbe  kwenye namba uliyotuma pesa na email yako na jina la kitabu na utatumia mara baada ya kutuma pesa yako. Majina yatatokea DEOGRATIUS KESSY unapotuma pesa kupitia simu yako.

MUHIMU; pata kitabu hiki kwa bei ya ofa kabla ya mwezi huu kuisha baada ya hapo bei itabadilika hivyo wahi mapema ujipatie nakala yako kwa bei ya ofa ya shilingi elfu tano tu, hakika hutojutia thamani ya maarifa utakayoyapata kwani ni zaidi ya shilingi elfu tano.

Mwisho, karibu sana rafiki tuweze kutanua wigo wa maarifa kwani hakuna  mtu maskini duniani bali kuna akili maskini na akili maskini nidyo chanzo cha matatizo mengi kwenye maisha yetu. Nakutakia kila la heri rafiki yangu.

Rafiki na Mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com

Asante sana

%d bloggers like this: