Nilichojifunza Kwenye Haya Maisha

Pale tunapokutana na changamoto au mambo hajaenda kama vile tunavyotaka sisi huwa kitu cha kwanza tunachofikiria ni nani amesababisha lakini huwa tunajisahau na sisi tumehusikaje kutokea kwa kile kilichotokea. Hata sisi wenyewe huwa tunachangia sana kwa changamoto mbalimbali katika maisha yetu lakini huwa hatukubali tunajiona sisi ni watakatifu. Kwenye kila kitu kinachotokea kaa chini jiulize …

Tunza Uadilifu wako

Uadilifu ni kuishi kile ulichoahidi na unachosimamia kwa mfano, umeahidi utakua mwaminifu katika maisha yako. Basi unaishi kile ambacho umekiahidi na ukienda kinyume maana yake umevunja uadilifu wako. Uadilifu wako una thamani kubwa kuliko almasi hivyo basi, usifanye chochote kile cha kuharibu uadilifu wako kwa sababu ukishauchafua ni vigumu kuusafisha. Umekula kiapo cha kuwa mwaminifu …

Tabia Inayowashinda Watu Wengi

Ni uaminifu. Watu wameshindwa kuwa waaminifu kwao wenyewe na kwa wengine. Uaminifu ndiyo mtaji unaolipa kwenye kila eneo la maisha yetu. Kuanzia kazi, mahusiano, biashara na nk. Kama kila mmoja angekuwa mwaminifu tu kwenye mambo madogo ambayo anajiwekea kufanya na angeyafanya basi dunia ingekuwa sehemu salama sana. Usiishi kwa kufuata mkumbo wa watu, kama watu …

Nawasaidia Lakini Hawana Shukrani

Ukiwa ni mtu wa kutaka kurudishiwa shukrani pale unaposaidia basi utaumia sana kisaikolojia. Waswahili wanasema shukrani ya punda ni mateke. Kazi yako kubwa iwe ni kufanya kazi yako na siyo kusubiri shukrani. Wewe toa bila kuwa na matarajio ya kupokea. Pata picha kuku anavyotimiza wajibu wake wa kutaga na kutoa mayai, ulishawahi kumuona akilalamika hata …

Tahadhari; Usikosee Wito Wako

Kukosea wito wako, ni sawa na mtu anayefanya kazi sana halafu haoni matokeo anayozalisha. Na hakuna kitu kigumu kama kujua wito wako, ukikosea wito ni kama vile umepotea njia. Kitu muhimu ambacho ningependa uondoke nacho hapa leo ni kwamba utafanikiwa zaidi iwapo utafanya kazi au biashara inayoendana na wito uliopo ndani yako. Achana na kufanya …

Usipofanya Kazi Yako Asili Itakuadhibu

Ukichunguza sababu halisi za watu kuwa hivyo walivyo leo wasababishi wakubwa ni wao wenyewe. Inawezekana ni uvivu, uzembe au ujinga ndiyo unamfanya mtu kubaki katika mkwamo au kuendelea kupata matokeo yale yale. Ujinga ni kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule halafu unategemea kupata matokeo tofauti. Kama hufanyi kazi yako vizuri, kwenye eneo lolote …

Usitawanye Nguvu Zako

Rafiki, jihusishe na kitu kimoja pekee na komaa na kitu hicho mpaka utakapofanikiwa au pale uzoefu wako unapokuonesha kwamba ni wakati wa kuachana nacho. Kwa mfano, kugonga nyundo kwenye msumari mmoja kwa kurudia rudia kunafanya msumari huo uingie ndani. Pale ambapo umakini wa mtu unawekwa kwenye kitu kimoja, akili yake inakuwa inamletea njia za kuboresha …

Watu Wengi Wamekosa Kitu Hiki Kwenye Maisha Yao

Leo asubuhi katika kipindi cha Billionaires in training, nimejifunza kitu kimoja kwamba watu wengi hawafanikiwi kwa sababu ya kukosa ustaarabu wa hali juu. Ni watu wachache sana katika jamii yetu ambayo wana ustaarabu wa hali ya juu, watu wamezoea kufanya kitu mpaka waambie kufanya. Ni kitu cha ajabu sana kwamba mtu anajua wajibu wake lakini …

Anzia Mahali Fulani

Kwenye maisha ili upate uzoefu wa kitu chochote kile, unapaswa kuanzia mahali fulani ili upate uzoefu. Ukienda sehemu wanakuhitaji utoe uzoefu wako juu ya kile unachofanya, hutakiwi kubaki unatoa macho tu, bali unatoa uzoefu wako kwa kile ulichowahi kufanya. Maisha siyo visingizio visivyokuwa na maana, bali ni kuonesha matokeo ya kile unachofanya au ulichofanya. Ili …

Sanaa Iliyosaulika Lakini Yenye Nguvu Kubwa

Kusikiliza kwa makini ni Sanaa Iliyosaulika lakini yenye nguvu kubwa sana ya ushawishi. Ndiyo maana una mdomo mmoja na masikio mawili, kwamba unapaswa kusikiliza zaidi kuliko kuongea. Watu wengi huwa ni waongeaji sana na kitu kinachowazuia wasiweze kuwajua wengine na kuwashawishi. Kwenye kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling, mwandishi …

Create your website with WordPress.com
Get started