Ukiona mtu anachukia mafanikio ya wengine jua kabisa hajui maana ya mafanikio kwake ni nini.
Mafanikio kwako yana maana gani?
Ukishajua mafanikio kwako yana maana gani huwezi kuchukia mafanikio ya watu wengine.
Mafanikio yana maana tofauti tofauti kwa kila mmoja wetu. Kwa kulijua hilo usichukie mafanikio ya watu wengine bali yapende.
Hakuna kitu kinawazuia watu kufanikiwa kama kuchukia mafanikio ya wengine. Ndiyo maana masikini wengi huwa hawawi matajiri kwa sababu wanawachukia matajiri wameaminishwa matajiri ni watu wabaya na wasiojali wengine.
Hutaweza kuwa na furaha kwenye maisha yako kama unachukia pale unapoona wengine wana furaha kuliko wewe.
Na hutafanikiwa kama kila aliyefanikiwa unamwona ni mbaya kwako.
Hatua ya kuchukua leo; Ili kuondokana na chuki hii ya mafanikio ya wengine kwanza hakikisha unajua mafanikio kwako yana maana gani kwa sababu mafanikio yanatofautiana kwa kila mtu.
Unachoona wengine wamefanikiwa ukipewa wewe kinaweza hata kisikufurahishe.
Kaa ukijua kuwa kila mtu anapambana na magumu yake, unaweza ukaona watu kwa nje ukasema wamefanikiwa sana ila ukipewa maisha yao na unaweza hata usiyapende na ukatamani maisha yako.
Furahia mafanikio ya watu wengine kwani unapofurahia na wewe utakuja kufanikiwa na kupiga hatua zaidi.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog