Kama Unataka Kwenda Mbinguni Epuka Kufanya Dhambi Hizi Hapa Mbili

Siko hapa kukuhubiria injili bali niko kukuambia vitu viwili tu ambavyo vinawakwamisha watu wengi kufanikiwa kwenye maisha yao.

Hata kwenda mbinguni ni mafanikio pia lakini siyo kila mtu ataenda mbinguni kwa sababu ya yale anayofanya.

Tabia ulizonazo na yale unayofanya unafikiri yatakufikisha kule unakotaka kufika?

Acha utani, weka kazi hakuna kitu kirahisi. Ingekuwa rahisi kila mtu angefanya na angefanikiwa. Maisha yanahitaji nidhamu ya hali ya juu na siyo sababu.

Watu wengi ni wazuri wa kutafuta sababu na siyo matokeo lakini, ni nani aliyebadilisha dunia kwa njia ya sababu? Hivi unafikiri wale ambao wameleta mapinduzi hapa duniani wangekuwa na sababu kama zako dunia leo ingekuwaje?

Epuka uvivu. Kiasili sisi binadamu ni wavivu. Watu wengi hawapendi kazi, hawapendi kujitesa, wanataka mafanikio makubwa bila kuweka kazi.

Wakati mwingine hata katika mambo ya kiimani, mtu unakuta ni mvivu hata kusali, mvivu hata wa kuamini.

Hivi unafikiri kwa dhambi tu ya uvivu unaweza kufanikiwa kwenye kitu gani?

Uvivu unawatafuna watu wengi, usipokuwa makini utajikuta kila siku utamaliza sababu. Na sababu huwa haziishi, watu wanataka kuona matokeo uliyozalisha na siyo sababu za kutokufanya kwako.

Acha dhambi ya uvivu, uvivu unawatafuna watu wengi. Vitu vingi unashindwa kufanya kwa sababu tu ya uvivu na siyo sababu halisi.

Uvivu unatembea na sisi kwenye kila eneo la maisha yetu, usipokuwa makini utajikuta unafanya mambo ambayo hayana maana kila siku.

Epuka uzembe. Uzembe ni dhambi mbaya katika karne hii ya ishirini na moja.

Usikubali kuwa mzembe, uzembe ni dhambi mbaya inayokuja kwa kufanya kimazoea, mtu anakuwa anajua anatakiwa kufanya nini ila anakuwa tu mzembe wa kutokufanya bila sababu.

Hebu fikiria ungekuwa unaambiwa ukifanya kitu fulani unapata hela unafikiri watu wasingefanya? Kwa mfano, kila atakayewahi kwenye kikao atalipwa kiasi fulani cha fedha, unafikiri kuna mtu angechelewa?

Kwenye maisha yangu sipendi mtu mvivu na mzembe. Napenda mtu ambaye anajituma kwa sababu mtu mvivu na mzembe anakuwa na maisha ya hovyo sana.

Mtu akishakuwa mvivu atashindwa kujitumikia yeye mwenyewe na wale wanaomzunguka.

Hatua ya kuchukua leo; epuka kuwa mzembe na mvivu ni dhambi mbaya katika maisha yako.

Chukia kutoka moyoni kuitwa mzembe na mvivu. Weka kazi kwenye mambo yako ili usiitwe mvivu na mzembe.
Ukiepuka dhambi hizi kwenye maisha yako hakika utafanya vizuri sana kwenye kila eneo la maisha yako hata mbinguni utaingia kwa sababu uzembe na uvivu unawakwamisha watu wengi sana kufanikiwa.

Wakati mwingine unatafuta sababu za kwa nini hufanikiwi lakini jibu linaweza kuwa ni kwa sababu ya uvivu na uzembe wako tu, kwa nini wewe ushindwe na wengine waweze?

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started