Design a site like this with WordPress.com
Get started

Naweza Kuajiri Watu Kunisaidia Kufanya Kila Kitu, Isipokuwa Vitu Hivi Viwili

Frank Bettger katika kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling aliweza kumnukuu na kujifunza kauli moja kutoka kwa aliyekuwa mmiliki wa viwanda alisema hivi, naweza kuajiri watu kunisaidia kufanya kila kitu isipokuwa vitu viwili tu, kufikiri na kufanya vitu kwa mpangilio wa umuhimu wake.

Rafiki yangu, huwa nakushirikisha hapa vitu vinavyofanya kazi kama kweli ukivifanyia kazi.

Unatakiwa katika maisha yako, utenge siku moja iwe siku ya kufanya mipango tu. Siku ya kupangilia wiki yako itakuwaje, unapangilia jumatatu utafanya nini, utakutana na nani na nk.

Kuna nguvu kubwa sana ya kukaa chini na kuipangilia siku yako kwani kadiri unavyotumia muda mwingi kupangilia mambo yako ndivyo unavyohitaji muda kidogo katika kutekeleza mipango hiyo.

Bila kuwa na mipango, hakuna kitu chochote kinachoweza kukamilishwa.

Ni bora kufanya kazi kwa ratiba kali siku sita za wiki na kuzalisha matokeo makubwa, kuliko kufanya kazi siku saba za wiki bila ya kuzalisha matokeo au kupiga hatua zozote zile.

Inasikitisha kweli kuona watu wanajiendea tu kimazoea, hawana mipango ya siku wala wiki, yaani wanaongozwa na matukio. Kama hujapangilia unataka nini unafikiri utawezaje kukitekeleza?

Hatua ya kuchukua leo; Vipe vitu hivi kipaumbele na utaweza kufanya makubwa
Kufikiri na kupanga.

Rafiki yangu, ni muhimu sana utenge muda wa kutosha kufanya vitu hivyo viwili, kupanga na kufikiri. Itakusaidia sana na kukuzalishia matokeo mazuri unayotaka kuyaona kwenye maisha yako.

Watu wengi hawataki kufikiri, kwa sababu kufikiri ni kazi ngumu ndiyo maana hawakai chini na kupanga.

Nenda kafikiri na kapange mpango wa wiki nzima inayokuja utakuwaje. Usiyakimbie maisha yako, kaa chini na yapangilie.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: