Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kila Wakati Kuwa Na Kitu Hiki

Kuwa na kitu cha kufanyia kazi.

Kila wakati kuwa na namba ambayo unapaswa kuifanyia kazi. Usikubali kuwa na maisha ambayo unakuwa na muda halafu huna kitu cha kufanyia kazi.

Kila wakati jipe kazi, jipe jukumu moja la kufanyia kazi na ukilimaliza jipe jukumu lingine tena.

Hakuna kupoa, ni kazi kazi. Siyo kwamba usiwe na muda wa mapumziko, kuwa na muda wa mapumziko lakini usikae muda mrefu pasipo kufanya kazi.

Usikubali kuwa karakana ya shetani, akili au mtu ambaye hajishughulishi anakuwa karakana ya shetani.

Pata picha unaamka umeipangilia siku yako, umekuwa na mpango kazi wako wa siku unafikiri utapata muda wa kuhangaika na yasiyokuwa na umuhimu kwako?

Hatua ya kuchukua leo;
Jipe namba za kufikia kwenye kila eneo la maisha yako.

Kwa mfano, kwenye eneo la fedha, chukua kipato chako unachopata sasa zidisha mara 10, namba utakayopata ndiyo kiwango chako sahihi ambacho unapaswa ukifanyie kazi mpaka ukipate.

Kwa namba hiyo akili yako haiwezi kulala, itafikiria namna ya kufikia malengo ya namba uliyojiwekea.

Habari njema ni kwamba mtu ambaye anakuwa na malengo ya kufanyia kazi anakuwa anafanikiwa na kujituma zaidi kuliko mtu ambaye hana hata malengo yeye anafanya ili mradi tu amefanya.

Upendo unaanza na kujipenda wewe mwenyewe kwanza, una mambo mengi ambayo unatakiwa kuyakamilisha na kutoyakamilisha maana yake hujipendi.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: