Design a site like this with WordPress.com
Get started

Kabla Mteja Hajanunua Bidhaa au Huduma Unayouza Lazima Kwanza Anunue Kitu Hiki Kutoka Kwako

Huwa tunafikiri katika mauzo wateja wanaanza kununua bidhaa zetu, kitu ambacho siyo sahihi.

Iko hivi rafiki yangu, kabla mteja hajanunua bidhaa au huduma Unayouza Lazima kwanza akununue wewe muuzaji.

Ili mteja akununue wewe muuzaji lazima kwanza muuzaji uwe unauzika. Muuzaji ukiwa hauuziki watu watakuwa hawana mpango hata wa kununua kile unachouza.

Unatakiwa uwashawishi watu kwa mwonekano wako mzuri.

Unatakiwa kuwa na nadhifu, vaa vizuri kwa kufanya hivyo mteja ataanza kununua wewe kabla hata ya kile unachouza.

Kitu kingine kinachopelekea watu waanze kukununua wewe kwanza ya kile unachouza ni uso wa tabasamu.

Utaweza kujiuza haraka kabla hata ya bidhaa unayouza pals tu unapokuwa na tabasamu.

Wachina wana msemo wao unaosema, kama huna uso wa tabasamu usifungue biashara au duka.

Je, wewe una uso wa tabasamu?

Wakati mwingine kinachokufanya usiuze ni kukosa uso wa tabasamu, unakuwa na kisirani muda wote, mteja anafika kwenye biashara yako wewe umenuna, unakuwa na uso wa mbuzi ambao hauna tabasamu, yaani uko “siriazi”
Unapokuwa ‘siriazi’sana unawajengea wateja wako hofu hata ya kuja kwenye eneo lako la biashara.

Lakini unapokuwa na tabasamu unapata faida nyingi mno.
Moja, watu watakuonea wewe ni rafiki yao unawajali kama utakua na uso wa tabasamu ukilinganisha na uso ambao hauna tabasamu.

Kitendo cha kutabasamu kina nguvu ya kukufanya ujisikie vizuri.

Unapokuwa na tabasamu ni rahisi kuwaambukiza wengine nao wakawa na tabasamu kama lako.

Kitu kingine ni kuwa na shauku, hakuna kitu kinacholipa duniani kama shauku. Ukiongea kwa shauku au kufanya kitu chochote kwa shauku KUBWA unakuwa unawashawishi watu kununua wewe kabla hata ya kile unachouza.

Hatua ya kuchukua leo; vaa uso wa tabasamu muda wote na kuwa mtu wa shauku KUBWA kwa sababu utawashawishi watu waanze kukunua wewe kabla ya kile unachouza.

Tunaweza kupata chochote kwenye maisha kama tutaweza kuuza zaidi. Kazana kuuza, maana mauzo ndiyo yanaleta mafanikio makubwa. Mauzo ndiyo yanaleta fedha mifukoni, bila mauzo hakuna maisha.

Habari njema ni kwamba, unapokuwa na tabasamu la kweli kwenye uso wako, unaonekana kuwa mtu mwenye bahati zaidi. Pata picha leo unavyokwenda kuwa mtu wa bahati zaidi kwa kuwa tu na uso wa tabasamu je, utajisikiaje kama leo utaongeza mauzo yako na kuwashawishi watu watu kwa kuwa tu na tabasamu?
Hata ukiongea na simu na mtu ukiwa na tabasamu unakuwa una ushawishi mkubwa kuliko ambaye hana tabasamu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: