Design a site like this with WordPress.com
Get started

Usitafute Huruma Kwa Watu Wengine

Ni kawaida yetu sisi binadamu pale tunapopitia changamoto mbalimbali zinazotukabili huwa tunaona ni vema na haki kutafuta huruma kwa watu wengine juu ya yale tunayopitia.

Tunafikiri kwamba, kwa njia ya kuwaelezea wengine matatizo yetu ili watuhurumie ndiyo tunaweza kutatua tatizo.

Pambana na hali yako, usitafute huruma kwa watu, kila mtu ana changamoto zake hivyo yakabili maisha yako.

Ukiwalalamikia watu kwamba huna hela, hali ngumu, unasomesha, watoto wanakusumbua, huna kazi hawatakusaidia kitu zaidi ya kujidharirisha tu, huna haja ya kutafuta huruma kwa wengine bali wajibika na maisha yako.

Maisha yako ni wajibu wako na changamoto zako ni wajibu wako.

Ishi katika mtazamo chanya kwamba, wewe ndiyo mkurugenzi wa maisha yako, hivyo unawajibika kwa chochote kile kinachotokea kwenye maisha yako kiwe kizuri au kibaya jua wewe ndiyo msababishaji mkuu.

Kila mtu akitafuta huruma, dunia itakua ya hovyo sana, lakini kila mtu akipambana na hali yake dunia itakua bora na sehemu salama ya kuishi kwa kila mmoja wetu.

Hatua ya kuchukua leo; usianike changamoto zako kwa watu kwa lengo la kutafuta huruma.
Kila mtu ana changamoto zake hivyo na wewe beba changamoto zako.

Hakuna mtu ambaye yuko duniani hapitii magumu, kila mtu ana magumu yake ila tu yanatofautiana.

Usitafute huruma kwa njia ya kueleza changamoto zako kwa watu ili usaidiwe. Wajibu wa maisha yako ni wako mwenyewe, wajibika na wewe uishi.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: