Miaka 200 Ijayo

Kuwa na kiasi kwenye maisha yako, haijalishi umefanikiwa kiasi gani miaka 200 ijayo huenda hakuna atakayejua hata kama uliishi hapa duniani. Kila unapoanza kujiona wewe ni muhimu kuliko wengine kumbuka kitakachotokea MIAKA 200 ijayo na dunia itakua imekusahau kabisa. Rafiki, ishi maisha yenye maana kwako na siyo maisha ya kujionesha na kutaka wengine waone wewe …

Jinsi Ya Kuondokana Na Wivu

Maana rahisi ya wivu ni kujiona wewe unastahili zaidi kuliko wengine. Sina uhakika kama itakufaa, na wivu ni wivu tu, hakuna wivu mzuri wala mbaya. Jinsi gani ya kuondokana na wivu? Usiwe na wasiwasi utapata majibu sahihi hapa. Kwanza ni rahisi sana, usijilinganishe na yeyote. Pili, kubali kwamba kuna watu watakaokuwa wamekuzidi kwa chochote unachofikiri …

Pata Picha Leo Unaacha Kuwa Hivi

Kama ulikuwa haujui, akili zetu sisi binadamu ni volkano ya maoni. Kwa nini? Kwa sababu tunapenda kuwa na maoni kwenye kila kinachotokea aidha tunakijua au hatukijui ndiyo maana ukiwaomba watu maoni hata hana atajilazimisha kusema tu maana asipofanya hivyo watu watamuonaje au watamchukuliaje. Wanafalsafa wengi wanatuambia siyo sahihi kuwa na maoni kwenye kila kitu. Kama …

Hiki Ni Kitu Cha Uhakika Kwenye Maisha Yako

Sina uhakika kama itakufaa lakini leo nina habari njema kwako rafiki yangu nikupendaye. Moja kuwa tayari kupoteza kila kitu. Na uwe uhuru kupoteza kila kitu wala usitetereke kwa kwenye maisha kuwa huru ina maanisha kuishi utakavyo na kupata unachotaka. Mbili, chochote kile ulichonacho kwenye maisha yako utakipoteza huo ni uhakika wala halihitaji ubishi. Hiyo ni …

Maisha Bora Ni Kufanya Vitu Hivi

Vitu tunavyofanya kwenye maisha yetu vina pande mbili; Moja raha naMbili maana. Tunasukumwa kufanya vitu kwa sababu labda vina raha kwetu kufanya au vina maana kwetu. Maisha bora ni kufanya vitu ambavyo vina raha na maana na siyo kuegemea upande mmoja pekee. Kuna wakati unahitaji kufanya vitu vya raha na ukijisikia kufanya hivyo fanya kwa …

Kabla Hujampenda Mtu Yeyote Mpende Kwanza Huyu

Jipende kwanza wewe mwenyewe. Mtu anayefanya vizuri kwenye eneo lolote lile ni yule ambaye anaanza kujipenda yeye mwenyewe kwanza. Unapojipenda wewe mwenyewe kwanza, itakulazimisha hata wale waliokuzunguka wawe bora na wajipende wao wenyewe. Kwa sababu, hatuwezi kuwabadilisha watu wawe vile tunavyotaka sisi pasipo sisi kuwaonesha kwa vitendo. Hatuwezi kuwapenda wengine kama sisi wenyewe hatujipendi. Falsafa …

Hiki Ndicho Kitakachopima Mafanikio Yako

Katika msingi wa falsafa ya ustoa unaamini kwamba dunia iko hivyo ilivyo yaani hakuna kitu kizuri wala kibaya na hakuna kitu kirahisi wala kigumu. Hapa tunajifunza kuwa, mtazamo wako ndiyo chaguo lako. Je, una mtazamo gani chanya kuhusu kufanikiwa kwenye maisha yako? Kwa mfano, wako ambao wanasema somo la hisabati ni gumu na wako ambao …

Jiwekee Ukomo

Kila kitu kinahitaji ukomo kwenye maisha yako.Na usipokuwa na ukomo kwenye vitu unavyojihusisha navyo utajikuta unachoka na kupoteza nguvu kubwa pia. Jiwekee ukomo kwenye vitu utakavyojihusisha navyo, jua ni maeneo gani uko vizuri na weka juhudi kwenye hayo, mengine yote achana nayo. Huhitaji kufanya kila kitu ndiyo ufanikiwe, unahitaji kufanya machache kwa ubora wa hali …

Utaishia Kuwa Hivi

Kama unafanya vitu ili wengine wakuone na kukusifia, nakuhakikishia kuwa utaishia kuwa mtumwa wa wengine. Acha kupima umuhimu wako kwa namna wengine wanavyokuchukulia, fanya kile kilicho sahihi kwako na usijali wengine wanasema au kuchukuliaje. Haya siyo maisha ya kujali sana watu wanasemaje, bali jiangalie wewe mwenyewe. Nataka kukuuliza swali? Unafikiri nani anayejali maisha yako?Nani anakosa …

Hii Ndiyo Sababu Inayokuzuia Usipate Kile Unachotaka

Kila mtu anapenda kupata kile anachotaka kwenye maisha yake lakini kipo kitu kimoja kinachochangia sana watu kutokupata wanachotaka. Utajisikiaje kama leo utakijua kile ambacho kinakuzuia usipate kile unachotaka? Pata picha maisha yako yatakavyobadilika pale tu utakapojua kile ambacho kinafanya usifanikiwe. Habari njema ni kwamba, unaweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, kama utaweza kuuza …

Design a site like this with WordPress.com
Get started