Design a site like this with WordPress.com
Get started

Rasilimali Yenye Uhaba Kwa Kila Mtu

Rasilimali yenye uhaba kwa kila mtu ni fedha.

Kila mtu ana uhaba wa fedha hilo halina ubishi, ndiyo maana kila siku mtu anajituma ili kuendelea kupata fedha zaidi. Ingekuwa haina uhaba basi watu wasingefanya kazi kwa sababu inapatikana kirahisi.

Angalia muda, ni rasilimali ambayo inaleta kila kitu kwenye maisha lakini haina uhaba watu wanatumia muda wao vibaya.

Pata picha rasilimali ya fedha na muda ipi ina uhaba kwako?

Kwa kuwa fedha ni rasilimali yenye uhaba, unatakiwa kuithamini pale unapoipata na siyo kuitumia vibaya.

Kitu kinavyokuwa na uhaba ndivyo thamani yake inazidi kupanda, hivyo unatakiwa na wewe upande kithamani.

Usipokuwa na vyanzo zaidi ya kimoja cha mapato ndiyo unatengeneza uhaba zaidi kwenye fedha. Ili kupunguza uhaba wa rasilimali hii na wewe ongeza kipato zaidi.

Hatua ya kuchukua leo; punguza uhaba wa kifedha kwenye maisha yako kwa kuongeza kipato zaidi.

Kitu cha mwisho rafiki yangu nikupendaye, kadiri unavyokuwa na akiba kubwa kifedha, ndivyo unavyoweza kujilinda na dharura mbalimbali zinazoweza kutokea.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: