Kutoka kwenye kitabu cha Tano za Majuma Ya Mwaka, kilichoandikwa na Kocha Dr Makirita Amani, kuna dhana ambayo nilijifunza katika eneo la fedha, nimeona ni vema na wewe nikushirikishe.
Karibu sana rafiki yangu,
“Kilio cha wengi kwenye fedha ni kwamba, watu wakipata fedha haikai na hata wakiweka akiba, haikai.
Yaani wakipata fedha au wakiwa na akiba matatizo ndiyo yanazaliwa, watu ndiyo wanapata shida na mahitaji ndiyo yanaongezeka.
Ni mpaka fedha walizonazo ziishe ndiyo matatizo yanatulia.
Kama unapitia changamoto kama hiyo, mwandishi anasema lipo suluhisho hupaswi kuendelea kuteseka rafiki yangu.
Mwandishi anasema, ukiwa na fedha akili yako inajua una fedha. Hivyo basi, ukikutana na chochote, hutaweza kuvumilia kama unayo fedha, utaitumia tu.
Sasa unapaswa kufanya nini?
Unachohitaji kufanya ni akili yako ijue kwamba huna fedha hivyo unapokutana na tatizo unalazimika kufikiria njia ya kulitatua na siyo kutumia fedha ulizonazo.
Katika kulazimisha dhana hii ya kujilazimisha kuishiwa kwanza unapaswa kuwa na bajeti yako ya kuendelea maisha .
Kisha tenga kipato kinachokidhi bajeti hiyo.
Kiasi kingine chote cha fedha kiweke kwenye akaunti maalumu ambayo huwezi kuondoa fedha hizo.
Kitu kingine cha ziada, kila fedha ya ziada unayopata ambayo hukuwa nayo kwenye ratiba, usitoe hata senti, yote weka kwenye akaunti hiyo muhimu.
Hatua ya kuchukua leo; jilazimishe kuishiwa pale matumizi yanapokuwa yako juu na kujikuta unatumia hela tu kununua vitu ambavyo hata ulikuwa huna mpango wa kununua kwa sababu tu una hela.
Habari njema ni kwamba, dhana hii itakusaidia uwe huna fedha kwa muda mwingi na inapotokea changamoto inayokuhitaji uwe na fedha, itabidi utafute njia nyingine za kupata fedha hiyo na siyo kutoa zile ulizoweka akiba kwa sababu umeweka sehemu ambayo huwezi kutoa.
Kitu cha mwisho cha kuondoka nacho hapa, jilazimishe kuishiwa na utaweza kuweka akiba, kuwekeza na kukuza kipato chako zaidi.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog