Ukiwa Na Hali Hizi, Epuka Kufanya Maamuzi

Kwenye kitabu cha the Baron letters kilichoandikwa na mwandishi Gary Halbart,  anamshirikisha  mtoto  wake  makosa  ambayo  amewahi kuyafanya kwenye  maisha  yake,  na  mengi aligundua  aliyafanya  akiwa  kwenye  moja  ya  hali  hizi nne.  Hivyo  anamwambia  mtoto  wake  asifanye  maamuzi  yoyote anapojikuta  kwenye moja  ya  hali  hizo  nne; Moja; hasira. Usifanye maamuzi ukiwa kwenye hasira, jisubirishe kufanya …

Inafanya Kazi Kwenye Kila Eneo La Maisha Yako

Kanuni kuu kwenye mauzo ni kwamba, ukijua kitu ambacho watu wanataka na ukawapa watakuwa tayari kukubaliana na wewe. Sheria hii siyo tu inafanya kazi kwenye mauzo, bali inafanya kazi kwenye kila eneo la maisha. Kwa kifupi rafiki yangu, tunaweza kusema ndiyo sheria kuu ya mahusiano ya binadamu. Pale unapomwonyesha mtu kitu anachotaka, atakuwa tayari kufanya …

Unaweza Kuwadanganya Mashabiki Lakini Siyo Watu Hawa

Biashara ni mchezo na wafanyakazi ndiyo wachezaji wenyewe. Na watu wa nje ni mashabiki tu. Sasa kama biashara ni mchezo, unaweza ukawadanganya mashabiki lakini huwezi Kuwadanganya wachezaji. Unaweza kuwadanganya mashabiki kuhusu mwenendo wa biashara yako, au familia yako, au kitu fulani kwa kuigiza kwamba mambo yanakwenda vizuri, lakini wale walio ndani wanajua kama mambo yanaenda …

Mabadiliko Yanaanzia Hapa

Katika familia, taasisi, kwenye biashara yako mabadiliko ya kweli kwenye jambo na eneo lolote lile huwa yanaanzia juu, yanaanzia kwenye uongozi na kisha yanasambaa kwa wengine. Samaki huwa anaanza kuozea kichwani, hii maana yake nini? Ukiona familia haiendi vizuri jua wazi wazazi ndiyo hawajasimama. Ukiona wafanyakazi wako wanaenda vizuri, jua uongozi wa juu UMESIMAMA. Wafanyakazi …

Jifunze Kwa Mtu Aliyepitia Magumu Na Akafanikiwa Ndoto Yake

Tabia huwa zinatengenezwa pale tunapopitia magumu. Katika magumu, ndiyo watu huwa wanatumia uwezo wao mkubwa uliopo ndani yao. Na uzuri ni kwamba hakuna mtu ambaye hana changamoto yaani yeye nyumbani kwake amebandika bango mlangoni kwamba hapa hakuna matatizo. Ulishawahi kuona nyumba ya namna hiyo? Kama hujawahi kuona, jua kwamba kila binadamu anapitia magumu yake. Leo …

Jinsi Ya Kuongeza Kiwango Chako Cha Utambuzi

Je, unajua kiwango chako cha utambuzi? Kabla hujaongeza kiwango chako cha utambuzi, unapaswa kwanza kujua au kupima kiwango chako cha utambuzi kikoje. Njia ya kupima kiwango chako cha utambuzi ni kwenye kujua majira ya siku.Hapo inakuwaje sasa?Ni rahisi sana, kwa mfano, bila ya kuangalia saa, sema muda ni saa ngapi yaani sema saa na dakika. …

Kosa Ambalo Wauzaji Wengi Huwa Wanalifanya Kwenye Biashara

Unaweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, kama utaweza kuuza zaidi. Ni kweli hilo halina ubishi, mauzo ndiyo kila kitu kwenye biashara na maisha kiujumla. Mauzo ndiyo moyo wa biashara, ambapo yanasukuma damu ya biashara ambayo ni fedha. Bila mauzo hakuna fedha kwenye biashara, na bila fedha hakuna biashara. Unaona hapo mauzo yalivyokuwa muhimu? …

Siri Namba Moja Ya Kupata Fedha

Kwenye kitabu cha The Baron letters, mwandishi Gary Halbert alimwandikia barua mtoto wake akiwa gerezani. Gary Halbert alikuwa mwandishi bora kabisa wa matangazo na hivyo alitumia muda wake kumshirikisha mtoto wake yale yote aliyojifunza kwenye maisha, kuanzia kuwa na afya bora, kupata nk. Hata wewe kama ni mzazi unaweza ukawa unaandika yale uliyojifunza na kumshirikisha …

Una Uhakika Wa Kufanikiwa

Sina uhakika kama itakufaa lakini ukichagua kitu kimoja au vichache ambavyo utavifanya kwa maisha yako yote, ukawa unajifunza kila siku na kuchukua hatua, halafu ukaachana na mengine yote wanayofanya wengine,Una Uhakika Wa Kufanikiwa. Watu wengi hawajatulia kwenye kitu kimoja, wamekuwa wanahangaika na kila jambo linalokuja mbele yao. Na mwisho wa siku wanakuwa wamechoka kweli lakini …

Ufunguo wa Kushindwa

Bill Cosby aliwahi kunukuliwa akisema, sijui ufunguo wa mafanikio ni upi, lakini ufunguo wa kushindwa ni kujaribu kumridhisha kila mtu. Sidhani kama nitakuwa na maneno mengine zaidi ya hayo. Ukitaka kushindwa kwenye maisha yako, basi jaribu kumridhisha kila mtu. Na ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako ishi vile utakavyo lakini usivunje sheria za asili na za …

Design a site like this with WordPress.com
Get started