Msingi ni huu; kila unapokuwa unahitaji fedha zaidi, jiulize swali hili, ni mtu gani naweza kumsaidia apate fedha zaidi?
Ukipata jibu, hapo ndipo mahali unapoweza kupata fedha zaidi.
Utaweza kupata fedha zaidi pale tu utakapomwezesha mtu mwingine kupata fedha zaidi.
Makosa makubwa ambayo watu wengi huwa wanayafanya kwenye kutaka kupata fedha zaidi ni kuangalia ni fedha za nani wanaweza kuzichukua.
Unafikiri ni kwa nini tumekuwa na wezi, matapeli na hata wapokeaji rushwa kwa sababu msingi wao kuhusu fedha ni kwamba, ili upate fedha lazima uzichukue kwa wengine na siyo kutoa thamani.
Hatua ya kuchukua leo; angalia kazi unayofanya na jiulize ni kwa namna gani huduma unayotoa au bidhaa unayouza inamwezesha mtu kupata fedha zaidi?
Angalia kile unachotoa au kuuza kinamwezeshaje mtu asipoteze fedha zaidi au aongeze kipato zaidi.
Ukiwa na mtazamo chanya kwenye fedha kwamba, kila mtu apate utafanikiwa sana kwani utaangalia thamani.
Ondoka na vitu viwili hapa ,angalia namna gani mtu anaweza asipoteze fedha zaidi au kuongeza fedha zaidi kwa kufanya hivyo kwa hakika kipato chako kitaongezeka.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog