Design a site like this with WordPress.com
Get started

Chukua Karatasi Yako Na Weka Sahihi Yako

Leo nataka kukuonesha ni kwa jinsi gani wewe uko tofauti na wengine na wakati mwingine nakushagaa pale unapotaka kuwa kama wengine badala ya kuwa kama wewe.

Pata picha unachukua kalamu na karatasi yako halafu unaandika saini yako. Kisha angalia saini yako inafanana na ya mtu mwingine yeyote hapa duniani?

Utajisikiaje kama hakuna mtu ambaye ana saini kama yako hapa duniani?

Hii itakua ni habari njema kwako kwamba dunia nzima hakuna mtu kama wewe lakini inasikitisha kweli kuona watu wanatumia muda wao mwingi kuwa kama wengine na siyo kupambana kuwa wao.

Ukiandika saini yako ulishawahi kuona ikifanana na mtu?
Ndivyo maisha yalivyo, kila mtu yuko kivyake, tuko tofauti sana.

Na jivunie vile ulivyo, usijali wengine wanakufikiriaje wewe jali kile unachotaka kwenye maisha yako.

Ishi maisha yako, usijali watu wanakuchukuliaje na siyo kazi yako kuhukumu mambo ya watu wengine.

Hatua ya kuchukua leo; usijilinganishe na mtu yeyote, wewe ni wa kipekee sana kama huamini nenda chukua kalamu na karatasi andika saini yako halafu muombe mtu wako wa karibu au mtu yeyote yule aweke saini halafu ufanye ulinganisho na utaona ni kwa jinsi gani hamfanani.

Siyo sahihi kwako kuwa kama wengine bali ni sahihi kwako kuwa kama wewe kwa sababu wewe ni mradi mkubwa sana ambao haujawahi kutokea hapa duniani.

Hivyo basi, kila mmoja wetu anapaswa kubaki na utofauti wake na tujifunze umuhimu wa kuwa sisi na siyo kuwaiga wengine.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: