Design a site like this with WordPress.com
Get started

Asante Ya Mtu Huyu Inapaa Mbinguni

Huwa tunafikiri kutafuta ufalme wa Mungu ni kusali na kuhudhuria kwenye nyumba za ibada mara nyingi.

Sina uhakika kama itakufaa lakini kutafuta ufalme wa Mungu ni pamoja na kusaidia watu wake.

Hata yule anayesali sana hajawahi kumuona Mungu kwa macho, ni katika kusaidia watu wake ndiyo tunamuona Mungu kwa macho.

Unaposaidia watu kupitia kile unachofanya, iwe ni kazi, biashara, huduma nk hiyo na ukawahudumia kile unachofanya kwa upendo wa dhati kabisa basi hiyo inakuwa sala inayopaa mawinguni.

Asante ya yule unayemhudumia ni nguvu kubwa ya kukufanya wewe uendelee kupiga hatua kuliko malipo unayopata au vyeo unavyopewa. Kwa mfano, mtu anaumwa ukamsaidia na akapona ile asante yake unakuwa umeshautafuta ufalme wa Mungu na kuutangaza.

Fanya kile unachofanya kwa upendo ni sala tosha itakayopaa mawinguni.

Pata picha ni watu wangapi wamekusaidia kwa mawazo, kwa maneno na vitendo na ni wangapi ulishawahi kuwaambia asante sana kwa kugusa maisha yako? Utajisikiaje kama leo utaanza kuwapa watu ASANTE ili uweze kuwafanya waendelee kupiga hatua?

Kama hakuna mtu anayejali, kuwa mtu wa kwanza kujali.

Hatua ya kuchukua leo; Sema Asante sana baada ya kufikia kwenye kilele cha huduma fulani.

Kila siku wanakuhudumia watu wengi je, unawapa asante?

Habari njema ni kwamba asante ya yule unayemhudumia ni nguvu kubwa ya kukufanya wewe uendelee kupiga hatua kuliko malipo unayopata au vyeo unavyopewa.

Kitu kimoja cha mwisho, kazi yako ni kufanya kazi bora na asante ya yule unayemhudumia ni sala inayopaa mawinguni.
Unamposaidia mtu, ona unashiriki katika kutafuta ufalme wa Mungu kwanza, na ufalme wa Mungu ndiyo watu wake.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: