Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hakuna Mtazamo Wa Hovyo Duniani Kama Huu

Kwenye kitabu chake jinsi ya kuuza chochote mwandishi Joe Girard anatuambia hakuna mtazamo wa hovyo duniani kama kuamini kwamba kitu hakiwezi kufanyika kwa sababu hakijawahi kufanywa.

Mtazamo huo ndiyo umewafanya wengi kushindwa kupiga hatua, kwa kuendelea na mazoea.

Hata kama hakuna mtu mwingine amewahi kufanya kitu fulani, kama umeona ndiyo unapaswa kukifanya ili kupata matokeo bora zaidi, basi kifanye.

Hivyo ndivyo ugunduzi mpya umekuwa unapatikana duniani, kwa watu kuwa tayari kujaribu vitu ambavyo havijawahi kufanyika.

Tafakari, kabla ya vitu ambavyo havijagunduliwa vilikuwepo mwanzo? Jibu ni hapana, nao wakifanikiwa kufanya na ikawezekana na wewe inawezekana.

Usiishi katika rejea za mitaani au za watu ambao hawajawahi kufanya makubwa halafu wanakuambia makubwa hayawezekani kwa sababu hayajawahi kufanyika.

Nenda kawe wa kwanza kufanya kama hakuna aliyewahi kufanya.

Usikubali kukatishwa tamaa na mtu ambaye hata maisha yake mwenyewe yamemshinda, waone wanaokuambia huwezi kama wapumbavu kwa sababu neno haiwezekani ni msamiati unaopatikana kwenye kamusi ya mpumbavu tu.

Hatua ya kuchukua leo; ondoa mtazamo hasi, amini kwamba kitu kinaweza kufanyika hata kama hakijawahi kufanywa.

Na ili kuwaonesha wengine kwamba mambo yanawezekana ni wewe kukamilisha kile ambacho wao wanasema haiwezekani.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: