Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ukitaka Kuharibu Mahusiano Yako Kuwa Mtu Wa Hivi

Kuna baadhi ya changamoto kwenye mahusiano huwa tunazinunua sisi wenyewe kwa kujitakia.

Sisi binadamu ni viumbe vya hisia, hivyo unapokuwa katika mahusiano na watu wengine jitahidi sana kuangalia hisia za watu.

Watu wanafanya maamuzi yao kwa hisia, na siyo kwa fikra.

Ukitaka kuharibu mahusiano yako na watu wengine kuwa mkosoaji.

Hakuna mtu anayependa kukosolewa.

Ukitaka kujenga ushawishi na kuimarisha mahusiano yako kuwa mtu wa kusifia na siyo kukosea.

Kwa mtu yeyote yule ambaye unahusiana naye huwezi kukosa kitu chochote cha kumsifia ambacho huwa anafanya vizuri.

Watu hawapendi kukosolewa, hivyo ukitaka kushindwa kwenye mahusiano kuwa mkosoaji.

Lengo letu sisi ni kuwa na mahusiano bora na wale wanaotuzunguka hivyo basi, badala ya kuwakosoa watu wasifie kwenye yale wanayofanya.

Hatua ya kuchukua leo; nenda kawasifie watu kwenye yale mazuri wanayofanya.

Kwa chochote kile kizuri ambacho umekiona kwa mtu msifie.
Usiwakosoe watu, utaharibu mahusiano yako, tafuta namna ambayo ataona ni namna gani amekosea yeye mwenyewe na siyo kumkosoa wewe mwenyewe.

Kitu kimoja cha mwisho cha kuondoka nacho hapa, usiwakosoe watu badala wasifie watu na ikiwa utafanya hivyo basi nakuja utajenga ushawishi na kukubaliana na watu wengi hivyo utafanikiwa sana kwenye kile wanachotaka.

Watu wakikukubali na mambo yako yataenda vizuri. Na ili mambo yako yaende vizuri basi wasifie watu badala ya kuwakosoa watu.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: