Vitu tunavyofanya kwenye maisha yetu vina pande mbili;
Moja raha na
Mbili maana.
Tunasukumwa kufanya vitu kwa sababu labda vina raha kwetu kufanya au vina maana kwetu.
Maisha bora ni kufanya vitu ambavyo vina raha na maana na siyo kuegemea upande mmoja pekee.
Kuna wakati unahitaji kufanya vitu vya raha na ukijisikia kufanya hivyo fanya kwa sababu unaishi mara moja tu.
Na kuna wakati unatakiwa kufanya vitu vya maana, na pale inapokubidi kufanya hivyo, basi fanya.
Hatua ya kuchukua leo; usiishi maisha ya kuegemea upande mmoja pekee.
Hivyo basi, maisha bora ni kufanya vitu ambavyo vina raha na maana na siyo kuegemea upande mmoja, kuwa na pande zinazokupa raha na maana.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog