Jipende kwanza wewe mwenyewe.
Mtu anayefanya vizuri kwenye eneo lolote lile ni yule ambaye anaanza kujipenda yeye mwenyewe kwanza.
Unapojipenda wewe mwenyewe kwanza, itakulazimisha hata wale waliokuzunguka wawe bora na wajipende wao wenyewe. Kwa sababu, hatuwezi kuwabadilisha watu wawe vile tunavyotaka sisi pasipo sisi kuwaonesha kwa vitendo.
Hatuwezi kuwapenda wengine kama sisi wenyewe hatujipendi.
Falsafa ya upendo, inatualika sisi tuanze kujipenda, kuwapenda wengine na tatu kupenda kile tunachofanya.
Pata picha ya maisha yako, je unajionaje? Unajipenda?
Ukijipenda utahakikisha unafanya kazi kwa juhudi na maarifa na utajitoa kweli ili uweze kupata vitu vizuri.
Inasikitisha kweli kuwaona watu hawajipendi, wanafanya kazi, biashara lakini wanaishi maisha ya shida ya kutojipenda.
Hatua ya kuchukua leo; anza kuishi falsafa ya upendo na hatua ya kwanza kabisa ni kuanza kujipenda wewe mwenyewe kwanza.
Iko nguvu kubwa sana katika upendo, usijidanganye kwamba unawapenda wengine na kile unachofanya lakini unajisahau wewe mwenyewe.
Wewe unatakiwa kujipa maslahi yako kabla ya wengine.
Hakikisha unakuwa bora kwanza kabla ya kuwawezesha wengine kuwa bora.
Chochote unachotaka kitokee kwa wengine kianze na wewe mwenyewe kwanza.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog