Design a site like this with WordPress.com
Get started

Pata Picha Leo Unaacha Kuwa Hivi

Kama ulikuwa haujui, akili zetu sisi binadamu ni volkano ya maoni.

Kwa nini? Kwa sababu tunapenda kuwa na maoni kwenye kila kinachotokea aidha tunakijua au hatukijui ndiyo maana ukiwaomba watu maoni hata hana atajilazimisha kusema tu maana asipofanya hivyo watu watamuonaje au watamchukuliaje.

Wanafalsafa wengi wanatuambia siyo sahihi kuwa na maoni kwenye kila kitu. Kama huna maoni usionee kusema sina maoni.

Kama huna cha kuongea, usiongee kaa kimya ni hekima pia.

Akili zetu ni volkano ya maoni, huwa hatukubali kupitwa bila kutoa maoni yetu.

Lakini, maoni mengi huwa siyo sahihi kwa sababu hatuna utaalamu wa yale tunayotolea maoni.

Pata picha leo unaacha kuwa mtu wa maoni kwenye kila kitu na hauogopi kusema huna maoni juu ya kitu fulani.

Utajisikiaje kama ukisema huna maoni?

Kama huna utaalamu kwa yale unayotolea maoni usione aibu kusema sina maoni.

Maisha yako yatakuwa bora kama utakua na maoni machache na tena kwenye yale maeneo ambayo una ubobezi nayo.

Hatua ya kuchukua leo; kwenye maeneo ambayo huna ubobezi usiogope kusema huna maoni.

Kitu cha mwisho rafiki yangu nikupendaye, maisha yako yatakuwa bora kama utakua na maoni machache na tena kwenye yale maeneo ambayo una ubobezi nayo. Kwenye maeneo mengine ambayo huna ubobezi nayo, usiogope kusema huna maoni.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: