Design a site like this with WordPress.com
Get started

Utaishia Kuwa Hivi

Kama unafanya vitu ili wengine wakuone na kukusifia, nakuhakikishia kuwa utaishia kuwa mtumwa wa wengine.

Acha kupima umuhimu wako kwa namna wengine wanavyokuchukulia, fanya kile kilicho sahihi kwako na usijali wengine wanasema au kuchukuliaje.

Haya siyo maisha ya kujali sana watu wanasemaje, bali jiangalie wewe mwenyewe.

Nataka kukuuliza swali? Unafikiri nani anayejali maisha yako?
Nani anakosa usingizi kwa sababu ya maisha yako? Hakuna kila mtu ana pambana na yake.

Ukishajifurahisha wewe mwenyewe,inatosha kwa sababu hakuna mtu anayekusaidia kulipa bili mbalimbali bali unajipambania mwenyewe sasa iweje ujali watu watakuchuliaje?

Ishi maisha yako, ishi mchakato wa maisha yako vizuri na watu watakuja kukuelewa vizuri kwenye matokeo mazuri.

Huna mtu mwingine anayejali zaidi ya wewe unavyojali.

Ishi uwezavyo ili mradi huvunji sheria za asili, nchi na maadili.

Fanya kitu ambacho ni sahihi kwako na acha kufanya vitu ili wengine wakuone.

Hatua ya kuchukua leo; acha kupima umuhimu wako kwa namna wengine wanavyokuchukulia.

Fanya kile kilicho sahihi kwako na usijali wengine wanasemaje au wanakuchukuliaje.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: