Njia Yenye Ushawishi Kwenye Kila Eneo La Maisha

Siyo njia nyingine bali ni nkia ya kuuliza maswali. Njia ya kuuliza maswali ina ushawishi kwenye biashara, kazi, huduma nk. Ukitaka kuwashawishi watu na kukubaliana na wewe, tumia njia ya maswali na siyo maelezo. Mara nyingi binadamu hapendi kuamuliwa, bali anapenda kuamua kupitia kuuliza maswali, yanamjengea fikra sahihi na kufanya maamuzi sahihi. Ukiwa katika mauzo …

Hiki Ndiyo Kinaweza Kukutofautisha Na Wengine Kwenye Biashara, Kazi Au Kile Unachofanya

Kinachoweza kukutofautisha na wengine wote ambao mnafanya biashara zinazofanana, kazi au huduma zinazoendana ni utoaji wa huduma bora sana kwa wateja. Kumbuka yoyote yule unayempatia huduma ni mteja wako. Jihoji tu, kuanzia kwenye biashara, kazi, mahusiano je, huduma ninayotoa hii kwa mteja wangu anaweza kuipata sehemu nyingine? Kama anaweza kuipata je, mimi natoaje huduma bora …

Usiwe Na Wasiwasi Na Kitu Hiki Hapa

Kabla hatujafanya kitu chochote kile, ndani ya nafsi zetu huwa kuna sauti tunazisikia. Wakati mwingine nafsi zetu zinatuambia hapa tunaweza au hatuwezi. Kinachowazuia wengi kufanikiwa ni kuwa na wasiwasi juu ya nafsi zao wenyewe.Mtu anataka ushindi wa kitu fulani, lakini hajiamini kabisa kama atashinda, kimdomo anasema anataka kitu fulani lakini nafsi haimaanishi. Kwa sababu walijaribu …

Usitawanye Nguvu Zako

Rafiki, jihusishe na kitu kimoja pekee na komaa na kitu hicho mpaka utakapofanikiwa au pale uzoefu wako unapokuonesha kwamba ni wakati wa kuachana nacho. Kwa mfano, kugonga nyundo kwenye msumari mmoja kwa kurudia rudia kunafanya msumari huo uingie ndani. Pale ambapo umakini wa mtu unawekwa kwenye kitu kimoja, akili yake inakuwa inamletea njia za kuboresha …

Kitu Pekee Kitakachokuwezesha Kuendelea Mbele

Kuna wakati unachoka na unaona ni sahihi kwako kuishia hapo ulipofika. Safari  ya  kupata  kile  unachotaka  kwenye  maisha  yako  haitakuwa  rahisi,  dunia haitakuachia  kirahisi ufanye  kila  unachotaka.  Utakutana  na  vikwazo,  changamoto  na magumu mbalimbali.  Kuna  wakati utajiona  kama  umekosea  kila  ulichokuwa  unafanya. Utafikia  hatua  ya  kukata  tamaa  na  kuona  haina  haja  ya  kuendelea  tena. Kitu  …

Mpe Mteja Uhakika Huu Hapa

Kwenye biashara au huduma yoyote ile unayotoa, unatakiwa kumpatia mteja  uhakika  wa  kile  unachomuuzia. Mfanye  ajisikie  kwamba  amepata suluhisho  na  siyo  kupoteza  fedha  zake. Siku  zote kutoa  fedha  kunauma,  kwa sababu  unapotoa  fedha  na  kulipia  kitu,  maana  yake  huna  tena  fedha  hizo  kwa matumizi  mengine.  Jua  mteja  wako  ana  matumizi  mengine  ya  fedha  zake, hivyo  …

Watu Wengi Wamekosa Kitu Hiki Kwenye Maisha Yao

Leo asubuhi katika kipindi cha Billionaires in training, nimejifunza kitu kimoja kwamba watu wengi hawafanikiwi kwa sababu ya kukosa ustaarabu wa hali juu. Ni watu wachache sana katika jamii yetu ambayo wana ustaarabu wa hali ya juu, watu wamezoea kufanya kitu mpaka waambie kufanya. Ni kitu cha ajabu sana kwamba mtu anajua wajibu wake lakini …

Anzia Mahali Fulani

Kwenye maisha ili upate uzoefu wa kitu chochote kile, unapaswa kuanzia mahali fulani ili upate uzoefu. Ukienda sehemu wanakuhitaji utoe uzoefu wako juu ya kile unachofanya, hutakiwi kubaki unatoa macho tu, bali unatoa uzoefu wako kwa kile ulichowahi kufanya. Maisha siyo visingizio visivyokuwa na maana, bali ni kuonesha matokeo ya kile unachofanya au ulichofanya. Ili …

Unafikiri Ni Nini Kinakuzuia Usifanikiwe?

Watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba kinachowazuia kufanikiwa ni vile walivyo. Lakini, ukweli ni kwamba, kinachokuzuia wewe usifanikiwe ni kile ambacho unajaribu kukikimbia.Kile ambacho unafikiria siyo ndicho kinachochukua muda na nguvu zako nyingi na kukuzuia kufanikiwa. Unachotakiwa kufanya ni, kujijua wewe ni nani, na unataka nini, kisha ukafanya maamuzi sahihi ya kuendesha maisha yako kwa kufanyia …

Sanaa Iliyosaulika Lakini Yenye Nguvu Kubwa

Kusikiliza kwa makini ni Sanaa Iliyosaulika lakini yenye nguvu kubwa sana ya ushawishi. Ndiyo maana una mdomo mmoja na masikio mawili, kwamba unapaswa kusikiliza zaidi kuliko kuongea. Watu wengi huwa ni waongeaji sana na kitu kinachowazuia wasiweze kuwajua wengine na kuwashawishi. Kwenye kitabu cha How I Raised Myself From Failure to Success in Selling, mwandishi …

Design a site like this with WordPress.com
Get started