Design a site like this with WordPress.com
Get started

Jiwekee Ukomo

Kila kitu kinahitaji ukomo kwenye maisha yako.
Na usipokuwa na ukomo kwenye vitu unavyojihusisha navyo utajikuta unachoka na kupoteza nguvu kubwa pia.

Jiwekee ukomo kwenye vitu utakavyojihusisha navyo, jua ni maeneo gani uko vizuri na weka juhudi kwenye hayo, mengine yote achana nayo.

Huhitaji kufanya kila kitu ndiyo ufanikiwe, unahitaji kufanya machache kwa ubora wa hali ya juu.

Ili ufanikiwe unapaswa kufanya mambo machache kwa ubora na siyo kufanya mambo mengi kwa viwango vya chini.

Jiwekee ukomo kwenye matumizi yasiyokuwa na ulazima kwenye upande wa fedha, mitandao ya kijamii na nk.

Kama yale unayoyapa muda mrefu na kuyafuatilia hayakupi mambo haya matatu achana nayo mara moja,
Hayakupi afya, utajiri na hekima.

Usijihusishe kabisa na vitu ambavyo vinakutenganisha na vitu vya maana. Kama ulevi unakutenganisha na mahusiano yako wewe na watu wengine acha, au yanakutenganisha na mambo ya kiroho acha kwa sababu hakuna faida unayopata.

Hatua ya kuchukua leo; jiwekee ukomo kwenye kila kitu unavyojihusisha navyo na jua ni maeneo gani uko vizuri na weka juhudi kwenye hayo maeneo ambayo unajua kabisa yanakusaidia.

Kabla sijamaliza napenda kukuambia kitu kimoja cha mwisho, kama vitu unavyojihusisha navyo havikupi afya, utajiri na hekima usijihusishe navyo kabisa na badala yake elekeza nguvu, muda na fedha zako kwenye vitu vya maana.
Ushabiki wa vitu ambavyo havikusaidii kulipa bili ni shetani kwenye karni hii tunayoishi, shabikia vitu vinavyokulipa tu na vingine viweke pembeni.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: