Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hii Ndiyo Sababu Inayokuzuia Usipate Kile Unachotaka

Kila mtu anapenda kupata kile anachotaka kwenye maisha yake lakini kipo kitu kimoja kinachochangia sana watu kutokupata wanachotaka.

Utajisikiaje kama leo utakijua kile ambacho kinakuzuia usipate kile unachotaka?

Pata picha maisha yako yatakavyobadilika pale tu utakapojua kile ambacho kinafanya usifanikiwe.

Habari njema ni kwamba, unaweza kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako, kama utaweza kuuza zaidi.

Kumbe basi, kinachofanya wewe usifanikiwe ni kwa sababu ya mauzo unayofanya.

Kama unauza kidogo, basi utapokea faida kidogo.

Sikufichi rafiki yangu nikupendaye, mafanikio makubwa kwenye maisha yako yamelala kwenye mauzo.

Kama unataka kufanikiwa kwenye maisha yako basi uza zaidi.

Jifunze namna ya kuuza zaidi kile unachofanya.

Kwenye ajira uza zaidi kile unachojua kwa ustadi wa hali ya juu, msaidie bosi wako kupunguza changamoto na siyo kuongeza changamoto kwa kufanya hivyo utaongeza thamani kubwa na bosi atakulipa zaidi, kwa mfano, gharama ambayo ameikoa atakuongezea wewe kwenye mshahara.

Ukiwa na biashara au huduma tafuta wateja wapya zaidi. Kuwa na wateja wengi wa kuwahudumia na kisha wapatie huduma nzuri sana.

Kwa wateja ulionao hakikisha mteja ananunua zaidi ili mauzo yaongezeke.

Ukiuza zaidi utapata faida zaidi.

Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako, nenda kauze zaidi.
Je, leo unakwenda kuuza nini zaidi?

Hivyo basi, maisha ni mauzo, kama hauuzi, ujue unauzwa kuwa makini kwenye hilo.
Ukawe muuzaji bora sana kuwahi kutokea duniani ili uweze kufanikiwa kwenye kile unachotaka kwenye maisha yako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: