Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ni Kitu Cha Uhakika Kwenye Maisha Yako

Sina uhakika kama itakufaa lakini leo nina habari njema kwako rafiki yangu nikupendaye.

Moja kuwa tayari kupoteza kila kitu. Na uwe uhuru kupoteza kila kitu wala usitetereke kwa kwenye maisha kuwa huru ina maanisha kuishi utakavyo na kupata unachotaka.

Mbili, chochote kile ulichonacho kwenye maisha yako utakipoteza huo ni uhakika wala halihitaji ubishi. Hiyo ni adhabu ambayo kila mmoja wetu amepewa mara tu baada ya kuzaliwa.

Tatu, hata maisha uliyonayo tu utayapoteza kwa sababu iko siku moja utakufa.

Nne, tumia vizuri kile ambacho unacho sasa hata siku moja kikichukuliwa hakitakuuma sana kwa sababu unajua ulikitumia vizuri.

Tano, uhuru kamili kwenye maisha ni kuwa tayari kupoteza kila kitu na bado maisha yako yasiterereke.

Sita, usijishikize kwenye vitu. Kwa sababu kinachowanyima wengi uhuru kamili kwenye maisha ni kujishikiza kwenye vitu ambavyo wanavyo.

Hatua ya kuchukua leo; pambana kupata chochote unachotaka, lakini kuwa tayari kwa wakati wowote kukipoteza na usiruhusu maisha yako yakavurugika.

Kitu kimoja cha mwisho rafiki yangu nikupendaye, chochote ulichonacho kwenye maisha yako umeazimwa kwa muda, hivyo kuwa tayari kunyang’anywa na kukirudisha kwa wenyewe.
Kuwa na njia mbadala kwenye kila eneo la maisha yako, usitegemee kitu kimoja kwenye maisha yako yaani kuwa na (back up).

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: