Design a site like this with WordPress.com
Get started

Hiki Ndicho Kitakachopima Mafanikio Yako

Katika msingi wa falsafa ya ustoa unaamini kwamba dunia iko hivyo ilivyo yaani hakuna kitu kizuri wala kibaya na hakuna kitu kirahisi wala kigumu.

Hapa tunajifunza kuwa, mtazamo wako ndiyo chaguo lako. Je, una mtazamo gani chanya kuhusu kufanikiwa kwenye maisha yako?

Kwa mfano, wako ambao wanasema somo la hisabati ni gumu na wako ambao wanasema hesabu ndiyo somo rahisi kumbe basi maisha ni mtazamo wako na unaiona dunia kadiri ya mtazamo ulioko ndani yako.

Ni kama vile mtu aliyevaa miwani, ukivaa miwani ya rangi nyekundu utaona vitu vya rangi nyekundu.

Louis Mann aliwahi kusema, kinachotokea kwa mtu siyo muhimu kama kinachotembea ndani yake.

Hapa tunajifunza nini? Tunajifunza kwamba, mtazamo ambao mtu anao ndani yake ndiyo unaamua mambo yawe kama mtazamo wake ulivyo.

Vipi tafiti nazo zinasemaje?

Tafiti za watu waliofanikiwa zinaonesha kwamba mtazamo unachangia asilimia 80 ya mafanikio na asilimia 20 ndiyo inachangiwa na vitu kama vile juhudi na maarifa.

Hii ina maana gani?

Maana yake mtazamo ni kufikiri kama mshindi. Kutegemea ushindi na kuwa tayari kushinda.

Hatua ya kuchukua leo;
Kuwa tayari kulipa gharama ya mafanikio makubwa.

Amua kwamba ni lazima ufikie mafanikio na kuamini unaweza kufanikiwa.

Hivyo basi, mara zote kuwa na matarajio chanya na kujiamini na kuwa na misingi mizuri ya kazi.

Kuwa na mtazamo chanya ambao unaendana na kile unachotaka kwenye maisha yako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: