Kuwa na kiasi kwenye maisha yako, haijalishi umefanikiwa kiasi gani miaka 200 ijayo huenda hakuna atakayejua hata kama uliishi hapa duniani.
Kila unapoanza kujiona wewe ni muhimu kuliko wengine kumbuka kitakachotokea MIAKA 200 ijayo na dunia itakua imekusahau kabisa.
Rafiki, ishi maisha yenye maana kwako na siyo maisha ya kujionesha na kutaka wengine waone wewe ni muhimu kuliko wao.
Hatua ya kuchukua leo; Kila unapotaka kufanya kitu ambacho siyo sahihi kufanya kwa mwenzako, jiulize miaka 200 ijayo nani atakua anakujua wewe?
Usipofanya mambo yenye maana, miaka 200 ijayo hakuna ambaye atajua hata kama uliwahi kuwepo.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog