Design a site like this with WordPress.com
Get started

Una Uhakika Wa Kufanikiwa

Sina uhakika kama itakufaa lakini ukichagua kitu kimoja au vichache ambavyo utavifanya kwa maisha yako yote, ukawa unajifunza kila siku na kuchukua hatua, halafu ukaachana na mengine yote wanayofanya wengine,
Una Uhakika Wa Kufanikiwa.

Watu wengi hawajatulia kwenye kitu kimoja, wamekuwa wanahangaika na kila jambo linalokuja mbele yao. Na mwisho wa siku wanakuwa wamechoka kweli lakini hawana matokeo mazuri waliyozalisha.

Lakini sasa wengi hawana uthubutu na nguvu ya kuepuka tamaa zinazopamba kwenye njia ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.

Acha kuhangaika na vitu vingi visivyokuwa na tija kwako. Hangaika na machache ambayo yanalipa tu. Muda na nguvu zako ni vitu vyenye ukomo, vitumie vizuri sana.

Hatua ya kuchukua leo;
Chagua kitu kimoja au vichache na vifanye kwa maisha yako yote huku ukiachana na mwingine.

Jifunze kila siku na chukua hatua.

Ukifanya hivyo, sina shaka wala wasiwasi na wewe ninakuhakikishia una uhakika wa kufanikiwa kwenye maisha yako kwa sababu umekaa katika mchakato sahihi.

Haijalishi una pata matokeo gani, kazi yako ni kukaa kwenye mchakato sahihi ili uweze kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Kila kitu kizuri kinakwenda kutokea katika mchakato sahihi.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: