Design a site like this with WordPress.com
Get started

Ufunguo wa Kushindwa

Bill Cosby aliwahi kunukuliwa akisema, sijui ufunguo wa mafanikio ni upi, lakini ufunguo wa kushindwa ni kujaribu kumridhisha kila mtu.

Sidhani kama nitakuwa na maneno mengine zaidi ya hayo. Ukitaka kushindwa kwenye maisha yako, basi jaribu kumridhisha kila mtu.

Na ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako ishi vile utakavyo lakini usivunje sheria za asili na za nchi na maadili ya jamii.

Usiwaogope watu bali waheshimu.

Fanya kazi zako kwa juhudi zaidi na utajitengenezea bahati zaidi.

Jua vizuri kile unachofanya na kifanye vizuri sana kuliko mtu mwingine yeyote.

Jijue wewe mwenyewe na tymia ubora wako kufanya makubwa.

Hatua ya kuchukua leo; ukitaka kufanikiwa kwenye maisha yako, fuata moyo na usijipe kibarua cha kutaka kumridhisha kila mtu.

Kazi ya kuwaridhisha watu ni kazi ambayo hakuna aliyewahi kushinda zaidi ya kupata hasara. Usikubali kuingia kwenye kazi ya kutaka kuwaridhisha watu maana utashindwa vibaya.

Mtu pekee ambaye unaweza kumridhisha ni wewe mwenyewe. Jiridhishe kwa kufuata moyo wako na ishi kwa kujiamini kwa sababu wewe ndiyo mkurugenzi wa maisha yako. Wewe ndiyo unajua kile unachotaka na si watu wengine.

Kama kitu ni sahihi wako fanya na kama kitu siyo sahihi usifanye. Na kama kitu kweli kwako sema na kama siyo kweli usiseme.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha  ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

Mwl. Deogratius Kessy

0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog

Leave a comment

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: