Usiweke Nukta Weka Koma

Kibinadamu inafikia mahali unachoka na kupelekea hata kukata tamaa ya kupata kile unachotaka kwenye maisha yako. Inafikia mahali unaweka nukta, unasema sasa basi hapa ndiyo umefikia mwisho. Njia za Mungu siyo zetu, kwenye maisha hakuna kukata tamaa, kikubwa ni kuendelea kukaa kwenye mchakato sahihi. Unaweza ukapoteza kila kitu, ukajiona uko njia panda na ukaweka nukta …

Hakuna Mfanyabiashara Anayeweza Kufanikiwa Kwenye Biashara Yake Bila Kujua Kitu Hiki Hapa

Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa kama haijui vizuri biashara yake kwa undani. Na changamoto ya watu wengi ya kutozijua biashara zao ni kwa sababu ya kushindwa kujifunza kwa vitendo na uzoefu. Hata kama umewaajiri watu wakusaidie kwenye kile unachofanya, hakikisha unakijua wewe mwenyewe vizuri sana na kwa undani. Unakuta hata waajiri wengi wanadanganywa na wafanyakazi wao …

Nawasaidia Lakini Hawana Shukrani

Ukiwa ni mtu wa kutaka kurudishiwa shukrani pale unaposaidia basi utaumia sana kisaikolojia. Waswahili wanasema shukrani ya punda ni mateke. Kazi yako kubwa iwe ni kufanya kazi yako na siyo kusubiri shukrani. Wewe toa bila kuwa na matarajio ya kupokea. Pata picha kuku anavyotimiza wajibu wake wa kutaga na kutoa mayai, ulishawahi kumuona akilalamika hata …

Tahadhari; Usikosee Wito Wako

Kukosea wito wako, ni sawa na mtu anayefanya kazi sana halafu haoni matokeo anayozalisha. Na hakuna kitu kigumu kama kujua wito wako, ukikosea wito ni kama vile umepotea njia. Kitu muhimu ambacho ningependa uondoke nacho hapa leo ni kwamba utafanikiwa zaidi iwapo utafanya kazi au biashara inayoendana na wito uliopo ndani yako. Achana na kufanya …

Sheria Namba Moja Ya Kushinda Na Kushikilia Kuaminika Na Wengine

Kwa dunia ya sasa hivi, uaminifu umekuwa ni bidhaa adimu, kamwe usitegemee kuipata kwa kila mtu. Uaminifu wa kitu chochote kile huwa unaanza na sisi wenyewe kwa mfano, Kama unapanga wewe mwenyewe halafu hufanyi hapo unakuwa siyo mwaminifu kwako mwenyewe. Ili uweze kuaminika lazima uwe na sifa za kuaminika. Mtu yeyote aliyejijengea sifa za kuaminika …

Usipofanya Kazi Yako Asili Itakuadhibu

Ukichunguza sababu halisi za watu kuwa hivyo walivyo leo wasababishi wakubwa ni wao wenyewe. Inawezekana ni uvivu, uzembe au ujinga ndiyo unamfanya mtu kubaki katika mkwamo au kuendelea kupata matokeo yale yale. Ujinga ni kufanya kitu kile kile kwa mtindo ule ule halafu unategemea kupata matokeo tofauti. Kama hufanyi kazi yako vizuri, kwenye eneo lolote …

Chochea Moto Huu Ili Uendelee Kuwaka

Unapaswa kuchochea moto wa hamasa uliopo ndani yako. Hamasa ni kama moto, usipouchochea huwa unazima. Ili moto uendelee kuwaka ,lazima uchochewe, kuwepo na nishati na hewa ya oksijeni. Vile vile kwenye hamasa, unaweza kuhamasika mara moja, lakini kadiri muda unavyokwenda hamasa hiyo inapungua. Unapaswa kuchochea hamasa yakko kila siku. Unapaswa kujikumbusha kule unakoenda na jinsi …

Usimpe Mtu Ahadi Ya Kuendelea Kutegemea Wakati Huna Uhakika Wa Kumpatia

Kwenye jamii zetu watu wamekuwa ni mabingwa wa kutoa ahadi na inafikia mahali ahadi zinawafunga watu na hata kukosa raha kwa sababu kila akiangalia amezungukwa na ahadi nyingi alizoamua kuahidi kwa hisia. Maisha ni yako na una uamuzi wa kutoa pale unapojisikia kutoa na siyo lazima. Usijifunge na ahadi, kama kitu huna uwezo nacho kutoa …

Usiwe Kopo Linaloelea Juu Ya Maji Likiwa Limefungwa

Ukichukua kopo la maji au chupa ya maji halafu ukaifunga na kuitupia kwenye mto, bahari, au ukaiweka bombani ikiwa imefungwa kamwe maji hayawezi kuingia ndani. Hii ina maana gani katika maisha yetu ya kawaida? Watu wengi huenda wanafanya kile wanachopaswa kufanya lakini hawapati matokeo mazuri yanayofanana na juhudi wanazoweka. Yaani wako kwenye maji lakini hawayafaidi …

Kama Unataka Kuuza Chochote Kile, Tafuta Kundi Hili

Kama unavyojua, maisha ni mauzo, lazima uuze kitu fulani ili upate fedha. Bila kuuza, ni wazi hakuna kipato utakachoingiza. Ili uweze kuuza chochote kile, unapaswa kutafuta kundi lenye njaa kali, kisha unawauzia kundi hilo chakula au kile wanachotaka ili kushibisha njaa yao. Nadhani unapata picha, mtu akiwa na njaa hasa, atanunua chakula kwa namna yoyote …

Design a site like this with WordPress.com
Get started