Katika familia, taasisi, kwenye biashara yako mabadiliko ya kweli kwenye jambo na eneo lolote lile huwa yanaanzia juu, yanaanzia kwenye uongozi na kisha yanasambaa kwa wengine.
Samaki huwa anaanza kuozea kichwani, hii maana yake nini?
Ukiona familia haiendi vizuri jua wazi wazazi ndiyo hawajasimama.
Ukiona wafanyakazi wako wanaenda vizuri, jua uongozi wa juu UMESIMAMA. Wafanyakazi hawawezi kuwa vizuri kama mmiliki hayuko vizuri.
Jambo lolote lile unalotaka kuliona linaenda kwenye eneo lolote lile, basi hakikisha juu wanakuwa vizuri.
Usitegemee mabadiliko makubwa chini wakati juu hakuna mabadiliko.
Anza mabadiliko na wewe mwenyewe kwanza, kisha watu wengine watajifunza kupitia wewe.
Kama uongozi unataka watu wabadilike, lakini wenyewe haubadiliki inakuwa vigumu sana mabadiliko kutokea.
Lakini mabadiliko yanapoanzia juu, chini nako kubadilika.
Hatua ya kuchukua leo; Kama unataka kuona mabadiliko chini kwa wale unaowasimamia, hakikisha mabadiliko hayo yanaanzia juu.
Kwa chochote kile unachotaka kukiona kwa upande wa uongozi, hakikisha mabadiliko hayo yanaanzia juu kwanza na kisha yatafuata chini.
MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.
Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.
Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.
Mwl. Deogratius Kessy
0717101505 au 0767101504
https://kessydeo.home.blog